Nini maana ya simu ya mkononi?
Simu ya mkononi ni kifaa kitumiacho umeme kinachoruhusu mawasiliano baina ya watu wawili au zaidi waliopo katika umbali tofauti wa kijiografia. Kifaa hiki huwawezesha watu kuwasiliana kwa sauti, maandishi, picha mgando pamoja na picha tembezi kutegemeana na uwezo wake.
Historia inaonesha kuwa simu ya kwanza ilitengenezwa na Mwanasayansi Martin Cooper mnamo mwaka 1973, akiwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Motorola, ambapo tarehe 3, Aprili 1973 aliweza kupiga simu kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo, simu za zamani zilikuwa kubwa na nzito sana, kiasi kwamba watumiaji hawakuweza kuziweka kwenye mifuko ya mavazi yao na zilikuwa na uwezo wa kupiga na kupigiwa tu. Baadae ziliboreshwa zaidi, zikawekewa uwezo wa kutuma na kupokea jumbe fupi za maandishi (SMS) pamoja na jumbe za picha (MMS), sambamba na kuzipunguzia ukubwa na uzito.
Maboresho yaliyofanywa katika simu za mkononi hadi sasa ni makubwa sana. Na hii inatokana na ushindani mkubwa uliopo baina ya watengenezaji wa simu, ambapo kila kampuni hupigana kwa kila namna ili kuleta bidhaa na huduma nzuri au bora zaidi sokoni.
Leo hii simu za mkononi zimeboreshwa zaidi ambapo, mbali na uwezo wa kupiga, kutuma SMS na MMS, pia, watumiaji wanafurahia vitu vipya na bomba zaidi, kama vile video Calls (sauti na kuonana baina ya watumiaji), mitandao ya kijamii pamoja na kuvinjari intaneti kwa kutumia simu zao.
Simu za kisasa zenye uwezo mkubwa zaidi na zinazompa nafasi ya kufanya mambo mengi zaidi mtumiaji kwa kitaalam zinaitwa SmartPhones na zile za kawaida zenye uwezo mdogo zinaitwa Feature Phones. Simu hizi za SmartPhone zinatumia program kuu ijulikanayo kwa kitaalam kama Operating System, inayofanya kazi ya kuendesha mfumo mzima wa simu kuanzia vifaa vinavyounda simu (hardware) pamoja na program ndogo ndogo (software).
Baadhi ya program zinazotumika sana kwenye simu za smatifoni ni pamoja na Facebook, WhatsApp, Youtube, Opera Min, Camera, BBM, Instagram, Bluetooth n.k. Kila program inafanya kazi tofauti na nyingine, japo kuna nyingine zinakaribiana katika matumizi na kila siku zinatengenezwa mpya.
Kwa sasa mahitaji na matumizi ya simu za smartphones ni makubwa sana, kwani watu wengi wanapeda kutumia simu hizo zinazorahisiha zaidi mawasiliano. Sababu nyingine ya watu wengi kuhitaji au kutumia smartphones ni urahisi wa kupata habari au taarifa za matukio mbalimbali kutoka pande zote za dunia. Mtu mwenye smartphone ana uwezo mkubwa wa kupata taarifa za aina mbalimbali kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Yawezekana hata wewe unayesoma chapisho hili, unasoma kwa kutumia smartphone yako.
Baadhi ya kampuni zinazotengeneza na kusambaza simu za Mikononi ni Apple, Samsung, Huawei, Lenovo, LG, Tecno, iTel, TCL pamoja na ZTE. Kampuni hizo zinatoa simu za aina zote (kubwa na ndogo).
Kwa miaka ya hivi karibuni kuna watengenezaji wa simu feki kutoka nchini china waliokuwa wakisambaza simu hizo feki, hususan barani Afrika. Simu hizo zilikuwa na madhara makubwa kwa watumiaji, hivyo baadhi ya nchi zimeshachukua hatua za kuzifunga simu hizo na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa katika zoezi hilo ambapo katikati ya mwaka uliopita, 2016 kulifanyika zoezi la kufunga simu feki.
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment