We Like Sharing

Sunday, January 8, 2017

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone mpya ya Android

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone mpya ya Android

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone mpya ya Android

Asante sana kwa kutembelea Blugu yetu hii ya Nzegamedia, inayokupatia habari za matukio mbalimbali pamoja na elimu ya matumizi ya simu za mikononi pamoja na kompyuta.

Leo hii nimekuandalia mambo kadha wa kadha msomaji wetu unayopaswa kufanya baada ya kununua simu mpya ya smartphone. Soma kwa makini sana kwani naimani yatakusaidia katika kuboresha maisha ya simu yako na kuifanya ibaki kuwa madhubuti kwa muda mrefu zaidi.

Tia chaji simu yako

Baada ya kuitoa simu yako mpya kutoka kwenye boksi lake, hakikisha unaiweka chaji kwa muda wa masaa matatu (3hrs) kabla ya kuanza kuitumia. Huu ni ushauri unaotolewa na watengenezaji wa simu za mkononi, kwa ajili ya kuifanya simu yako iwe inakaa na umeme kwa muda mrefu zaidi.

Unapotia simu yako waweza kuizima, au kama utaiacha ikiwa imewaka, hakikisha unaiweka katika silent mode au Flight Mode. Pia unashauriwa usiitumie kwa namna yoyote simu yako wakati ikiwa inaingiza umeme.

Pangilia simu yako

Baada ya kuitia chaji simu yako hakikisha unaweka sawa mipangilio ya simu yako. Miongoni mwa mipangilio unayopaswa kuifanya kwenye smartphone yako mpya ni kama ifuatavyo:
  1. Lugha ya simu
    Mara nyingi simu za smartphone huja na lugha ya kiingereza, kwa hiyo unaweza kuchagua lugha nyingine unayoona inafaa zaidi kwa ajili ya kurahisisha utumiaji wa simu yako.
  2. Saa na Tarehe
    Ni muhimu pia kupangilia saa katika simu yako, kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukukumbusha muda pamoja na kuruhusu programu zinazohitaji muda sahihi kwenye simu kufanyakazi. Kuna programu nyingine haziwezi kufanyakazi kama simu yako haijapangiliwa vizuri saa ya mfumo wa simu na Whatsapp ni mfano wa Applikesheni zinazohitaji mpangilio sahihi wa muda.
  3. Themes/muonekano
    Pia ni muhimu kuweka sawa themes unazopendelea ili simu yako iwe na mvuto zaidi machoni mwako. Hii inahusisha pia kubadili au kuweka Wallpapers au picha inayokaa mbele ya kioo cha simu yako. Unaweza kuchagua wallpapers zinazokuja na simu (default wallpapers) au waweza kuchagua picha zako binafsi kwenye gallery. Pia hakikisha unapunguza mwanga wa kioo cha simu yako (display light/brightness) ili kuepusha kuharibu/kuumiza macho yako.
  4. Mobile Data/Handset configurations
    Data/Handset configuration ni maneno ya kitaalam yanayomaanisha kuipangilia simu yako ili iweze kutumia vifurushi vya Internet na kukupa nafasi ya kuwasiliana na watumiaji wengine wa internet kupitia mitandao ya kijamii na tovuti za kawaida.

    Kwa hiyo ni muhimu kufanya mipangilio ya APN sahihi kutegemeana na mtandao wa simu za mkononi unaotumia, kama vile Airtel, Vodacom, Zantel, Halotel, Tigo, n.k. Bila data configurations huwezi kutumia mitandao ya kijamii na intaneti kwa ujumla.

Fungua akaunti ya Google/Playstore/Martket

Baada ya kupitia hatua zote za juu kwa usahihi ni muhimu pia kutengeneza Akaunti ya Google Playstore itakayokuwezesha kufungua Playstore au Marketplace, ambazo ni applications zinazokupa uwezo wa kupakua Applications (.apk), Movies pamoja na Michezo mbalimbali ya kwenye simu.

Ingiza au sasisha (update) Programu/aplikesheni kwenye simu yako

Baada ya ku kuhakikisha intaneti inafanyakazi kwenye simu yako, pamoja na kufungua Akaunti ya Playstore, sasa weza kuingiza Aplikesheni mpya au waweza kuzisasisha (update) zile ulizozikuta kwenye simu yako mpya.

Mara nyingi simu za android huja zikiwa na baadhi ya program lakini program hizo huwa zimeshapitwa wakati kwa hiyo tunakushauri uzi-update ili zipokee mabadiliko mapya kutoka kwa watengenezaji wa Apps husika (Apps Developers).

Playstore ina Applications nyingi sana zenye matumizi tofauti. Zipo Apps kwa ajili ya kuchati (Facebook, Imo, Facebook, whatsApp, Instagram, n.k.) pamoja na Apps za kupakua videos/movies au audio/muziki. Pia zipo Apps zilizotengenezwa kwa ajili ya kupiga picha (camera), pamoja na apps za kuvinjari intaneti kama vile Chrome, Opera Mini, UC Browser, n.k.

Pakua Apps kadri ya mahitaji yako, ila nakushauri usipakue zisizo na umuhimu kwako na usipakue Applications usizozijua matumizi yake au utendaji wake kwani kuna program nyingine zaweza kuharibu simu yako (Malware).

Dhibiti Matumizi ya umeme kwenye simu yako

Simu za smartphone zinatumia umeme mwingi sana ukilinganisha na simu za kawaida kwa sababu zina kioo kikubwa sana na processors zake ni kubwa pia. Kwa hiyo ili kuepusha kumaliza umeme haraka kuna mambo kadhaa yafuatayo yatasaidia:
  1. Punguza mwanga wa simu (brightness)
    Hii husaidia kwa kiasi fulani kupunguza matumizi ya umeme kwenye simu yako hivyo kuifanya simu yako kukaa kwa muda mrefu bila taabu ya kuishiwa chaji.
  2. Zima GPS, Bluetooth pamoja na Data connection
    Hakikisha unafunga/kuzima GPS, Bluetooth pamoja na Mobile Data au Wi-fi pale unapokuwa huzitumii. Kumbuka pia kuwa unapowasha vitu hivyo simu hutumia umeme mwingi sana, hivyo kama utaviacha viwe hewani muda wote itapelekea simu yako kuisha chaji haraka sana sambamba na kuua betri ya kifaa chako. Tunapendekeza zoezi hili liwe endelevu.
  3. Ondoa vibration kwenye simu yako
    Vibration ni feature iliyopo kwenye simu nyingi ambayo endapo mtumiaji ameiruhusu kufanya kazi, hufanya simu itetemeke, na wakati huo simu hutumia umeme mwingi sana. Tunakushauri uweke milio ya kawaida badala ya vibration ili uepushe simu yako kuisha chaji haraka na kuifanya betri yako kudumu.

Weka screen Guard/protector

Screen Guards au protectors ni karatasi za plastiki zilizotengenezwa kwa ajili ya kuzuia vioo cha simu visikwaruzike na kuleta mwonekano mbaya. Screen protectors hufanya simu yako kuwa na muonekano mzuri na kuepusha simu kuchakaa hususan sehemu ya kioo. Baadhi ya wauzaji wa simu huwawekea kabisa wateja wao pale wanapouza simu zao za smartphones, ila ikitokea umenunua simu na hujapatiwa screen protector itabidi ununue ili uipe maisha marefu zaidi simu yako.

Weka Screen Locks (Patterns, Pins, n.k)

Unapotumia simu yako mara nyingi unafanya mawasiliano ambayo ni ya siri sana kiasi kwamba hupendi watu wengine wayajue. Na wakati mwingine unaweza kuitumia simu yako kuhifadhi taarifa zako binafsi ambazo si vizuri watu wengine kuziona.

Habari njema ni kwamba watengenezaji wa simu za mikononi wanaliwekea kipaumbele swala la kulinda taarifa binafsi za wateja wao zisivuje, kwa hiyo kuna feature huambatanisha kwenye mifumo ya simu inayomruhusu mmiliki wa simu husika kuweka passwords, patterns, au PIN (personal Identification Numbers) ambazo huzitumia kufungua simu.

Ukiweka screen lock ni kwamba kila unapohitaji kufanya kazi yoyote kwenye kifaa chako, utaambiwa uingize, neno la siri la kufungulia simu, hivyo kama mtu mwingine atachukua au kuokota simu yako itakuwa vigumu kuifungua kama atakuwa haifahamu password uliyoweka.

Screen lock ni mbinu ya kwanza ya kulinda simu za mkononi pamoja na taarifa zake, lakini unaweza kuingiza Apps nyingine zinazoweza kulinda simu yako pamoja na Data zako.

Hitimisho

Siku zote hakikisha unajua namna ya kuitunza simu yako ili uipe maisha marefu zaidi. Vya kuzingatia ni zile mbinu za kulinda betri isiishiwe umeme haraka, kuweka screen guards pamoja na ile ya kuweka screen locks/passwords.

Somo linalofuata linahusu Data/Handset configuration. Katika somo hilo utajifunza namna ya kufanya mipangilio sahihi ya Internet hususan APN (Accress Point Names). Kumbuka kila mtandao wa simu za mkononi una settings/mipangilio yake binafsi inayotofautiana na kampuni nyingine na aina ya simu, lakini sisi Nzegamedia tutajitahidi kukupatia elimu ya handset configurations za mitandao na simu zote.

Related Articles

Kulazimisha simu isome 3G tu

4G LTE ni nini?

3G ni nini na inafanyaje kazi?

2G ni nini na inafanyaje kazi?

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment