We Like Sharing

Monday, November 21, 2016

Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi

Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi

Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi

Kigoma, Tanzania

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, mkoani Kigoma, kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mheshimiwa Moses Joseph Machali, leo ameamua kuhamia rasmi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo yameelezwa kwenye taarif aliyoitoa Mbunge huyo wa zamani wa Kasulu Mjini ambapo ametaja sababu nyingi zilizopelekea kuchukua maamuzi hayo ya kuhamia CCM. Miongonzi mwa sababu zilizomfanya ahamie Chama Cha Mapinduzi, ni pamoja na kuona mwelekeo mzuri wa uongozi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Bw. Machali amesema, kwa muda mrefu alikuwa akishirikana na viongozi wenzake kutoka vyama vya upinzani hususani, NCCR na ACT Wazalendo, kupinga ufisadi uliokuwa unafanywa na viongozi wa serikali bila kuchukuliwa sheria stahiki.

Machali aliwataja Rais Dkt. John Pombe Magufuli na waziri mkuu wa Tanzania, Bw. Majaaliwa kuwa wanaonyesha dhamira dhati ya kuijenga nchi ya Tanzania.

"Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli". Alisema Bw. Machali.

Aidha, Bw. Machali alisema kushughulikiwa kwa viongozi wanaokiuka taratibu na kupunguza au kuzuia matumizi ya fedha yasiyo ya lazima, ni miongoni mwa sababu zilizomfanya aukubali uongozi na mwenendo wa serikali ya Rais Magufuli.

Bw. Machali alieleza kuwa kilichokuwa kinawafanya wapige kelele wapinzani ni pamoja na uongozi wa serikali ya awamu zilizotangulia kuwa na dhaifu wa kutowachukulia hatua viongozi waliokuwa wanabainika kuhusika katika ufisadi wa mabilioni ya fedha za wananchi.

"Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini". Alieleza Bw. Joseph Machali.

Aidha, Bw. Machali alisema anawashangaa viongozi wa Upinzani wanaoendelea kupinga jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli.

Kwa upande wa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wamesema hawawezi kupinga maamuzi yake, na wamempokea kwa moyo mmoja, na hatua nyingine zitafuata kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi kwa Wanachama wapya.

"Sisi kama chama cha mapinduzi tunaheshimu uamuzi wake na hatua ya pili kumpokea kwenye chama katiba za kikanuni zitafuatwa na hasa ukizingatia mimi namfahamu ni mtu mwenye msimamo, kwahiyo naheshimu maamuzi yake na hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa katiba na kanuni zetu za chama kuwapokea wananchama wanaoingia katika chama chetu kutoka upande wa vyama vingine”. Amesema Bw. Ole Sendeka, msemaji wa Chama Cha Mapinduzi.

Bw. Machali alikuwa Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini, kwa tiketi ya Chama cha NCCR (2010 - 2015). Baadae alijiunga na ACT Wazalendo, na leo amehamia CCM.

Bofya hapa kusoma taarifa nzima aliyoitoa leo Machali kwa vyombo vya habari

Picha ya Ole Sendeka, Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment