We Like Sharing

Saturday, November 19, 2016

Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi

Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi

Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi

Zanzibar, Tanzania

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amezindua wodi Mpya ya Watoto na Wazazi katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo mjini Unguja, visiwani Zanzibar.

Katika uzinduzi huo Dr. shein aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuwekeza na kuongeza bajeti yake ya kila mwaka katika sekta ya afya na elimu kwa kutambua kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanaletwa kwa nguvu kazi yenye afya bora na yenye elimu.

Dr. Shein alisema uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wake wa ahadi ya kuifanya hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya Rufaa, na ujenzi wa Wodi hizo ni umelenga kupunguza vifo vya watoto na akina mama vinavyotokana na uzazi na sababu nyinginezo.

Katika uzinduzi huo, pia Dr. Shein alisema serikali yake itaendelea kuitekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kutoa huduma za afya bure kwa wazazi visiwani humo.

Aidha, Dr. Shein alikishukuru Chuo Kikuu cha Haukeland na Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana katika ujenzi wa jengo jipya la watoto pamoja na kuweka vifaa vipya.

Pia, Dkt Shein alitumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya afya kutoa nafasi za ajira kwa wote wenye utayari wa kufanya kazi popote ndani ya visiwa vya Unguja na Pemba kwa mujibu wa mkataba wa ajira.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kutekeleza kwa kasi ahadi zake alizowaahidi wananchi wa Zanzibar.

Uzinduzi wa Wodi za watoto na wazazi, Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar.

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment