Dr. Shein awaonya watakaothubutu kuvuruga amani visiwani Zanzibar
Unguja, ZanzibarRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ametoa onyo kwa watakaosababisha kuvurugika kwa amani visiwani Zanzibar.
Hayo ameyasema alipokuwa anahotubia wanachama wa CCM katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 39 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika Kisiwandui, makao makuu ya chama hicho mjini Unguja.
Dr. Shein alisema, kumekuwepo na tetesi za kuwepo kwa watu ambao wana malengo ya kuvuruga amani visiwani humo, na amewaambia wananchi wasiwe na hofu kuhusu mipango hiyo, kwani serikali imejipanga vizuri kukabiliana na watakaohusika katika uharibifu au uvunjifu wa amani.
Akizungumzia kuhusu suala la kurudiwa kwa uchaguzi mkuu visiwani humo, Dr. Shein alisisitiza kuwa uchaguzi utafanyika mwezi machi mwaka huu, kama ilivyoamriwa, na amewataka wazanzibari wenye vigezo vya kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowahitaji, kuanzia Rais, Madiwani pamoja na wawakilishi.
Pia amewataka wananchi wapuuze ushawishi wa kususia kupiga kura siku ya uchaguzi unaofanywa na viongozi wa upinzani, hususan CUF.
“Wao wanashawishi wanachi kutokupiga kura, sisi tunawashawishi wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi hususan wafuasi wa CCM kwa ajili ya kupiga kura…” Amesema Dr. Ali Mohamed Shein.
Ikumbukwe kuwa kurudiwa kwa uchaguzi visiwani Zanzibar kumekuja kutikana na uchaguzi uliofanyika tarehe 25, Oktoba 2015 kufutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mh. Jecha Salim Jecha, kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na vitendo vilivyokiuka taratibu za uchaguzi ikiwemo kuwepo kwa kura nyingi zaidi ya watu waliojiandikisha kupiga kura.
Uchaguzi huo wa marudio unatarajiwa kufanyika tarehe 20, machi mwaka huu visiwani Zanzibar, licha ya Chama cha Civic United Front (CUF) kutoa tamko la kutokushiriki katika uchaguzi huo.
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment