We Like Sharing

Saturday, November 19, 2016

Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam

Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam

Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam

Dar Es Salaam, Tanzania

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Bw. Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku kumi (10) ndani ya jiji la Dar Es Salaam.

Katika ziara hiyo, Bw. Makonda amelenga kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakazi wa jiji la Dar Es Salaam ambapo leo ikiwa ni siku ya kwanza, ziara hiyo imeanzia Wilayani Kigamboni.

Mapema leo, mkuu huyo wa mkoa alizungumza na viongozi wa wilaya ya kigamboni kabla ya kuingia mitaani kuwasikiliza wananch juu ya kero wanazokumbana nazo. Akizungumza na viongozi hao, Makonda alisema ameamua kufanya ziara hiyo mahsusi kwa ajili ya kubaini kero za wananchi sambamba na kuwahamasisha watumishi wa serikali kuwatumikia wananchi.

"Nataka wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii ili kwenda sambamba na kasi ya Rais wetu". Alisema Makonda.

"Nimegundua asilimia 80 ya wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi, asilimia 80 ya watumishi wa umma hawafanyi kazi, ni wapiga majungu, wasoma magazeti - ni wambea. kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara". Aliongeza Makonda.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa aliwaambia viongozi kuwa hataki kufuatwa na wananchi wakitafuta msaada wa kutatua matatizo yao wakati chini yake kuna wasaidizi lukuki.

Katika ziara hiyo, Bw. Makonda alishuhudia uharibifu wa mazingira wilayani Kigamboni unaosababishwa na uchimbaji holela wa kokoto, hivyo alimtaka mkuu wa wilaya hiyo pamoja na vyombo vya ulinzi kuhakikisha wanashughulikiwa wale wote watakoonekana kuendelea kuchimba kokoto katika maeneo hayo.

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda akizungumza leo na vijana wa Sober House iliyopo Vijibweni jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda leo akikagua maeneo yaliyoharibiwa kutokana na uchimbaji holela wa kokoto, Mjimwema jijini Dar Es Salaam.

Habari nyingine zaidi...

Mkutano wa Maalim Seif Sharif Hamad Mtwara wazuiliwa

Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi

Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii

Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu

Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao

Sikiliza ngoma kali za Mangwea

Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa

Hotuba ya Dkt. Hamisi Kigwangalla, alipopokelewa Jimboni Nzega Baada ya Kutangaza nia Kugombea Urais wa Tanzania

Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016

Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump

Uchafu wa miji nchini Tanzania ni tishio kwa afya za wananchi wanaoishi katika miji hiyo

Makontena 11,884 na magari 2019 yapitishwa bandarini bila tozo

Upanuzi wa barabara ya MwanaKwerekwe hadi Fuoni, Zanzibar

Dr. Shein awaonya watakaothubutu kuvuruga amani visiwani Zanzibar

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment