We Like Sharing

Saturday, November 19, 2016

Mkutano wa Maalim Seif Sharif Hamad Mtwara wazuiliwa

Mkutano wa Maalim Seif Sharif Hamad Mtwara wazuiliwa

Mkutano wa Maalim Seif Sharif Hamad Mtwara wazuiliwa

Mtwara, Tanzania

Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad, leo alialikwa kama mgeni rasmi kuhudhuria mkutano wa ndani wa chama uliopangwa kufanyika Mjini Mtwara. Mkutano huo uliandaliwa na Jumuiya ya Vijana ya CUF(JUVICUF) Mtwara Mjini na bahati mbaya polisi wameingilia kati na kuzuia mkutano huo.

Taarifa za awali zilisema mkutano huo ulipangwa kufanyika leo majira ya saa tano asubuhi kwenye ukumbi uliopo katika chuo cha Stella Maris (Stemmuco) Mtwara mjini. Katika hali ya kushtukiza polisi walionekana kuzunguka katika mji wa Mtwara na wengine walisimama kwenye lango la kuingilia chuoni hapo, kitendo kilichoashiria kuzuiliwa kwa mkutano huo. Magari kadhaa ya polisi yalionekana katika eneo la chuo likiwemo gari moja lenye maji ya kuwasha.

Taarifa za Mkurugenzi wa Habari, uenezi na uhusiano wa Umma CUF, Bw. Mbarala Maharagande, zinasema mkutano huo ulilenga kukagua shughuli za chama, kupata maoni na mapendekezo kutoka kwa wanachama juu ya namna ya kuboresha utendaji wa chama kwa ngazi ya chini.

Aidha, taarifa zinadai kuwa jeshi la polisi lilipokea barua ya maombi ya Jumuiya ya Vijana ya CUF(JUVICUF) na kuijibu wakiruhusu Mkutano huo ufanyike. Pia jana Polisi walikabidhiwa barua ya Katibu Mkuu wa CUF (Maalim Seif) kwenda kwa IGP na ma RPC Lindi na Mtwara akiwajulisha juu ya ziara yake.

Leo asubuhi baada ya Maalim Seif kutua mjini Mtwara, Polisi walikwenda na magari yao katika chuo cha Stella Maris na kuwafukuza watu waliokwenda kuhudhuria mkutano huo, na baadae polisi waliwapa CUF barua ya kubatilisha ruhusa ya kufanya mkutano.

Picha ya Maalim Seif Shair Hamad na wafusi wengine wa CUF mara baada ya kutua mtwara mapema leo hii

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment