We Like Sharing

Saturday, November 19, 2016

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii

Dar Es Salaam, Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa wenyeviti wawili wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii na mmoja wa chuo.

Walioteuliwa na mheshimiwa Rais ni pamoja na Mhandisi Alhaji Mussa Iyombe amabye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Pia Rais Magufuli amemteua Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi, Faustine Karani Bee, kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF).

Wa tatu katika uteuzi huo ni Prof. Tadeo Andrew Satta ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Awali, Prof Tadeo Andrew Satta alikuwa anakaimu nafasi hiyo kabla ya uteuzi.

Picha ya ikulu ya Tanzania, Dar Es Salaam

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment