We Like Sharing

Monday, November 21, 2016

Ziara ya RC Paul Makonda jijini Dar yaibua makubwa

Ziara ya RC Paul Makonda jijini Dar yaibua makubwa

Ziara ya RC Paul Makonda jijini Dar yaibua makubwa

Dar Es Salaam, Tanzania

Leo ikiwa ni siku ya tatu kati ya siku kumi za ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Bw. Paul Makonda, ziara hiyo imeonesha kuibua mengi makubwa yaliyojificha. Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa katika ziara hiyo ya jiji zima ni pamoja na suala la uombaji wa rushwa unaofanywa na askari wa jeshi la polisi katika wilaya ya Temeke.

Wakiongea kwa uchungu mbele ya RC Makonda maeneo yaKeko, wananchi hao walivitaja vituo vya polisi vilivyokithiri kwa rushwa kuwa ni pamoja na Chang'ombe, Makangarawe na Kilwa. Wananchi walisema, wamechoshwa na vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi wilayani humo, ambapo askari wanawanyanyasa wananchi kwa kuwaomba rushwa, kuwabambikizia kesi pamoja na kuwakamata raia wasio na hatia.

Miongoni mwa wananchi waliowahi kukumbana na manyanyaso ya jeshi la polisi wilayani Temeke ni Fatma Said, ambaye alilalamika mbele ya Makonda, kuwa kijana wake ambaye ni Dereva wa Bodaboda alikamatwa na kisha pikipiki yake kuchukuliwa kituo cha polisi, ambapo pamoja na kufuatilia na kutii masharti aliyopewa, pikipiki hiyo hakuipata.

Mama huyo alsema, kijana wake aliambiwa na askari polisi waliomkamata atoe Tsh. 200,000 kama faini, na alitoa lakini hakupewa pikipiki hiyo na Fatma alipofuatilia aliambiwa atoe Tsh. 400,000 akatoa, lakini naye hakufanikiwa kupewa pikipiki hiyo.

"Pamoja na kutoa fedha hizo kijana wangu hakupewa pikipiki, nilipofuatilia niliambiwa nipeleke sh.400,000 na kadi, nikapeleka lakini sikupewa pikipiki hadi leo hii". Alisema Fatma. "Hii ni haki?” alihoji Fatuma.

Mkaazi mmwingine wa eneo hilo, alipaza sauti yake akidai kuwa askari polisi wa eneo hilo hukamata raia wasio na hatia na kuwapeleka katika vituo vya polisi, kisha huwaomba fedha ili waweze kuwaachia huru.

"Mkuu wa mkoa tunaomba uchunguze hili. Tunanyanyswa sana. Tunakamatwa bila hatia. Vituo vya polisi Chang’ombe, Makangarawe na Kilwa vimekithiri kwa rushwa na unyanyasaji wa raia.Chunguza utabaini ukweli”. Alisema kijana huyo akidai kuwa amewahi kukamatwa mara kadhaa na akskari polisi bila hatia.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda, baada ya kusikia kero hizo alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa Maalum wa Temeke, Gires Muloto, kutoa majibu juu ya tuhuma hizo, ambapo Muloto alisema atashughulikia kikamilifu askari wote wanaokwenda kinyume na sheria ikiwemo kujihusisha na vitendo vya rushwa na unyanyasaji.

Aidha, Mkuu wa Operesheni Maalum mkoa wa Dar es Salaam, Lucas Mkondwa, ameagiza wananchi kumpelekea majina ya polisi wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ameahidi kuwa sheria itachukua mkondo wake.

RC Makonda alionekana kukerwa na vitendo vya askari polisi hao wanaowanyanyasa raia wasio na hatia, na amewashauri wananchi kutengeneza mtego wa kuwanasa askari hao ikiwa ni pamoja na kuwarikodi kwa kutumia simu za mkononi na kisha kutuma taarifa hizo katika mamlaka husika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dr Es Salaam, Paul Makonda akiongea na wakaazi wa Keko

Habari nyingine zaidi...

Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii

Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA

Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar

Taarifa aliyoitoa Moses Joseph Machali kuhusu kuhamia Chama Cha Mapinduzi

Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi

Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu

Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao

Sikiliza ngoma kali za Mangwea

Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa

Hotuba ya Dkt. Hamisi Kigwangalla, alipopokelewa Jimboni Nzega Baada ya Kutangaza nia Kugombea Urais wa Tanzania

Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016

Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment