We Like Sharing

Saturday, November 19, 2016

Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Dar Es Salaam, Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 18 Novemba, 2016 alimteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw. Diwani Athuman kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Pia Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za Serikali kama ifuatavy:

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016

Pili, Rais Magufuli amemteua Dkt. Jones A. Kilimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na amemteua Bw. Sylvester M. Mabumba kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Prof. Patrick Makungu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO). Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Nne, Rais Magufuli amemteua Bw. Martin Madekwe kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi. Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Tano, Rais Magufuli amemteua Prof. Raphael Tihelwa Chibunda kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI). Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Taarifa hii ilitolewa jana tarehe 18/11/2016 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa.

Picha ya ikulu ya Tanzania, Dar Es Salaam

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment