We Like Sharing

Tuesday, December 29, 2015

Upanuzi wa barabara ya MwanaKwerekwe hadi Fuoni, Zanzibar

Upanuzi wa barabara ya MwanaKwerekwe hadi Fuoni, Zanzibar

Upanuzi wa barabara ya MwanaKwerekwe hadi Fuoni, Zanzibar

Zanzibar

Picha inayoonyesha Jengo la ghorofa lililopo
Fuoni karibu na kituo cha polisi.

Kama siku nyingi hujapita barabara ya kutoka Mwanakwerekwe hadi Fuoni mjini unguja, ukienda leo au siku zijazo utashangaa mabadiliko ya mandhari uliyokuwa umezoea kuyaona kipindi cha nyuma.

Ni katika harakati na jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) za kuboresha huduma za usafiri kwa raia wake mjini unguja, ambapo imeamua kupanua na kuboresha barabara ya kutoka Mwanakwerekwe hadi fuoni.

Mnamo tarehe 26/12/2015 Team ya Bongolike ilitembelea maeneo hayo na kujionea hali halisi juu ya namna ujenzi wa barabara hiyo unavyokwenda kwa kasi.

Ujenzi wa barabara hiyo unakwenda sambamba na ubomoaji wa nyumba zilizokuwa zimejengwa ndani ya himaya ya barabara hiyo. Wakitoa maoni yao kuhusu ujenzi wa barabara hiyo wananchi waliokuwa katika maeneo hayo walisema, upanuzi wa barabara hiyo utasaidia kupunguza msongamano wa magari uliokuwa unasababishwa na idadi ya magari kuongezeka siku hadi siku mjini humo.

"Kwa upande wangu nahisi hii itapunguza foleni za magari barabarani... unajua kila uchwao watu wananunua magari, kitu kinachopelekea Unguja kuwa miongoni mwa miji yenye magari mengi hususani kwa barabara hii iendayo maeneo ya shamba, kwa hiyo hii itapunguza foleni zisizo za lazima..." Alisema mmoja wa wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.

"Pia upanuzi huu utasaidia kuepusha usumbufu wa kupishana kwa wenye vyombo, maana hii iliyopo kwa sasa ni nyembamba ukilinganisha na idadi ya vyombo vya usafiri..." Aliongezea mwingine.

Picha inayoonyesha moja kati ya nyumba zilizobomolewa maeneo ya Taveta, mjini Unguja.

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

1 comment:

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/serikali-kuanzishwa-wakala-wa-uvuvi-tanzania-kwa-mwaka-2020.1647202/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-nyimbo-tuwapongeze-wasanii-hawa-kupelekea-utamu-wa-siasa-2020.1652542/

    https://www.jamiiforums.com/threads/wizara-ya-viwanda-na-biashara-ipo-kwenye-mchakato-wa-kuanzisha-wakala-wa-shopping-malls-tanzania.1647285/

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kimataifa-vipaumbele-vya-kujenga-reli-na-fursa-za-kibiashara.1647668/767 494826

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kwenye-mzishi-na-ukweli-kuwa-marehemu-alikuwa-anafanya-kazi-sana-na-pengo-lake-haliwezi-zibika.1652710/

    ReplyDelete