We Like Sharing

Tuesday, December 29, 2015

Alikiba mchizi wa bongo

Alikiba mchizi wa bongo

Alikiba mchizi wa bongo

Alikiba ni msanii wa muziki wa Bongo Flavour kutoka nchini Tanzania. Alizaliwa mnano Novemba 26, mwaka 1986, na amejizolea umaarufu mkubwa, si Afrika Mashariki tu, bali pia hata Afrika nzima na nje ya Afrika.

Alianza kutikisa ulimwengu wa muziki mnamo mwaka 2007 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Cinderella. Singo ya Cinderella ilimtambulisha Alikiba kwa wapenzi wa muziki hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, kutokana na maudhui yaliyomo katika nyimbo hiyo pamoja na sauti na midundo yake.

Nyimbo ya Cinderella ilihiti kiasi cha kukamata nafasi ya kwanza katika vipindi vya Top 10 na Top 20 kwenye vituo mbalimbali vya redio, ndani na nje ya Tanzania.

Baadhi ya nyimbo za Alikiba zilizomo kwenye albamu yake ya kwanza ni pamoja na Cinderella, iliyobeba jina la Albamu. Nyingine ni Msela, Yatima, Zaidi yangu, Nakshi nakshi Lagatoni na MacMuga.

Baadhi ya nyimbo zilizompatia na zinazoendelea kumpatia umaarufu Alikiba ni pamoja na Cinderella, Naksh Naksh, Njiwa, Usiniseme, Dushelele, MacMuga, na Everything. Nyingine ni Mwana, Chekecha Cheketua na Nagharamia.

Ali Kiba amewahi kupiga show nyingi sana ughaibuni hususani Ulaya, Marekani na Uarabuni, na amewahi kunyakua tuzo mbalimbali zikiwemo za Kili Music Awards za hapa hapa nyumbani, Bongo.

Mbali na uimbaji, Alikiba pia ni mtunzi/mwandishi mzuri wa nyimbo, Dancer, producer na Muigizaji pia. Pia amewahi kuombwa kusajiliwa na timu za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi, lakini alikataa kutokana na mapenzi yake makubwa kuegemea kwenye muziki.

Nyimbo za Ali Kiba zinazochezwa zaidi kwa sasa kwenye vituo vya redio nchini ni pamoja na Mwana, Chekecha Cheketua pamoja na Nagharamia alizozitoa hivi karibuni.

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

1 comment:

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/serikali-kuanzishwa-wakala-wa-uvuvi-tanzania-kwa-mwaka-2020.1647202/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-nyimbo-tuwapongeze-wasanii-hawa-kupelekea-utamu-wa-siasa-2020.1652542/

    https://www.jamiiforums.com/threads/wizara-ya-viwanda-na-biashara-ipo-kwenye-mchakato-wa-kuanzisha-wakala-wa-shopping-malls-tanzania.1647285/

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kimataifa-vipaumbele-vya-kujenga-reli-na-fursa-za-kibiashara.1647668/767 494826

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kwenye-mzishi-na-ukweli-kuwa-marehemu-alikuwa-anafanya-kazi-sana-na-pengo-lake-haliwezi-zibika.1652710/

    ReplyDelete