We Like Sharing

Friday, November 18, 2016

Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump

Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump

©2016. Bongolike! Designed by Chris Kabeya De Pro

Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump

Marekani

Donald Trump alizaliwa mnamo mwaka 1964 jijini New York katika familia ya kitajiri ya Bw. Fred Trump na mkewe Mary Ann Macleod. Utajiri wa Trump unatokana na mali aliyorithi kutoka kwa wazazi wake.

Trump alijiingiza rasmi kwenye siasa mwaka 2015 alipoamua kuwania kugombea kwa nafasi ya urais wa Marekan kupitia tiketi ya chama cha The Republican. Safari ya Trump katika kuwania nafasi ya urais ilionekana kuwa ya kimiujiza baada ya kuibuka mshindi akimbwaga mgombea wa kike kupitia chama cha Democratic, Bi Hilary Clinton.

Alipotimiza umri wa miaka 13, wazazi wake walimpeleka katika shule ya kijeshi walikoamini Trump angeweza kulelewa na kuwa mtu mwenye maarifa na elimu nzuri. Trump alipenda kumsaidia baba yake katika biashara baada ya kutoka shuleni. Alikabidhiwa kampuni ya baba yake mnamo mwaka 1971 ambapo baadae alibadilisha jina la kampuni na kuitwa The Trump Organization

Baada ya hapo Trump alihamia Manhattan ambako alifanikiwa kuimarisha uhusiano mzuri na watu wa maeneo hayo wenye nguvu zaidi.

Mnamo mwaka 2011, Trump alionyesha kuwa na mashaka juu ya taarifa kuwa Obama Obama ni raia wa Marekani. Obama aliamua kukiweka wazi cheti chake cha kuzaliwa 2011, kwa ajili ya kuuthibitishia ulimwengu kuwa yeye ni mzaliwa halali wa Marekani. Pamoja na Obama kuonesha sehemu aliyozaliwa, Donald pia hakupendezwa na Obama kuchaguliwa kuwa Rais, kwa sababu hakuvutiwa na sera zake, hivyo aliendelea kumshambulia Rais Obama kila alipopata nafasi ya kuzungumza.

Mwezi juni 16, 2015, Donald Trump alifufua matumaini yake ya kuwa Rais wa Marekani, na alitangaza nia ya kuwania kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha The Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani.

"Nawania rasmi kiti cha Urais wa Marekani, na tunakwenda kurudisha hadhi tena hadhi ya nchi yetu" Alisema Bw. Trump siku ya kujitangaza rasmi kuwania nafasi ya urais. "Mungu aliniumba kuwa Rais mwenye kutoa nafasi nyingi za kazi". Aliongeza. "Mipango yangu ni kuanza na usalama wa nyumbani, kwa maana ya Ujirani mwema pamoja na kuweka ulinzi madhubuti mipakani dhidi ya ugaidi". Aliwaambia wafuasi wake. "Bila taratibu na sheria, hakuwezi kuwa na amani na usalama. Tutajenga ukuta mkubwa, kwa ajili ya kudhibiti uhamiaji holela pamoja na uingizwaji wa madawa ya kulevya katika jamii zetu". Aliongeza Rais mteule, Bw. Trump.

Katika uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka huu Trump aliibuka mshindi akimbwaga Bi Hilary Clinton. Bw Trump alijizolea kura 278 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya ABC News. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe. Bw Trump alishinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News

Picha hizo hapo chini zinaonesha utajiri wa Donald Trump

Utajiri wa Bw. Dolnald Trump, Rais mteule wa Marekani
Utajiri wa Bw. Dolnald Trump, Rais mteule wa Marekani
Utajiri wa Bw. Dolnald Trump, Rais mteule wa Marekani

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment