Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa
MarekaniRais mteule wa Marekani, Bw. Donald Trump amesema hataki kupokea mshahara wa urais wa USD 400, 000 atakapoingia madarakani rasmi hapo january mwakani. Hayo aliyabainisha alipokuwa anafanya mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.
Bw. Trump alisema badala ya kupokea kiasi cha $400, 000 kama mshahara wake wa urais, atapokea $1 kwa mwaka mzima.
"Sijawahi kuzungumzia hili, lakini jibu langu ni hapana". Alisema Bw. Trump. "Nafikiri inanibidi kupokea kwa mujibu wa sheria $1, kwa hiyo nitapokea 1$ kwa mwaka". Aliongezea rais mteule Bw. Trump.
Ndugu msomaji, ikumbukwe pia kwamba dola moja ya kimarekani (1 USD), ni sawa na Tsh. 2200 za kitanzania, kwa hiyo kama Trump atasimamia msimamo wake huo atakuwa anapokea Tsh. 2200.
Aidha, taarifa nyingine zinasema kuwa Trump si kiongozi wa kwanza nchini marekani kukataa mshahara wake, bali kuna viongozi wengine pia ambao kwa nyakati na nafasi tofauti waliwahi kukataa mishahara yao. Viongozi hao ni pamoja na Herbert Hoover, aliyekuwa ametajirika kupitia biashara ya madini kabla ya kuingia madarakani, na John F Kennedy, aliyerithi utajiri mwingi, wote walikataa kupokea mishahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie wasiojiweza katika jamii.
Wengine ni Meya wa zamani Michael Bloomberg, gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger na gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney, nao pia walikataa kupokea mishahara yao.
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment