Tanzania na China kuendeleza ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama
Dar Es Salaam, TanzaniaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 novemba 2016 amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli na Jenerali Changlong wamefanya mazungumzo juu ya uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya Ulinzi na Usalama ambapo kumekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA).
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimwambia Jenerali Fan kuwa anathamini mchango wa serikali Jamhuri ya watu wa China wa kuimarisha Jeshi la Wananchi Tanzania, na amemuomba afikishe salamu na shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping.
Dkt. Magufuli amemhakikishia Bw. Fan kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha majeshi ya ulinzi na masuala mengine ya maendeleo.
Kwa upande wake Jenerali Changlong amempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli kwa uongozi wake mzuri na imara aliouonesha na ameahidi kuwa China itaendeleza uhusiano na ushirikiano baina yake na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi na usalama hususan kuimarisha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Habari nyingine zaidi...
Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar
Taarifa aliyoitoa Moses Joseph Machali kuhusu kuhamia Chama Cha Mapinduzi
Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi
Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Sikiliza ngoma kali za Mangwea
Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa
Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment