Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
NzegaKatika harakati zake za kutatua changamoto ya uhaba wa maji jimboni mwake, Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini, Mh. Hussein Mohamed Bashe, leo aliwakutanisha wataalamu wa maji, wenyeviti wa mitaa, wadau wa maendeleo pamoja na maofisa wake kwenye kikao kilichokuwa mahsusi kwa ajili ya kupeana taarifa juu ya muendelezo wa mradi wa maji wa muda mfupi pamoja na ule wa muda mrefu (ziwa viktoria).
Sambamba na kikao hicho, wajumbe wa kikao hicho wakiongozwa na maofisa wa mbunge, walifanya ziara kwenye eneo la uzalishaji maji, lililopo katika mtaa wa Uchama, kaskazini mwa mji huo wa Nzega.
Ziara hiyo hasa ililenga kuwapa elimu ya ufahamu wajumbe wote kama viongozi ambao wapo karibu na wananchi ili waweze kufikisha taarifa na ufahamu huo kwa wananchi juu ya jitihada zinazofanywa na mbunge wao katika kushughulikia tatizo la uhaba wa maji mjini hapo.
Ikumbukwe pia kuwa Mh. Bashe amekuwa akipigania upatikanaji wa maji jimboni mwake, na katika ziara ya kwanza ya Mh. Rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli mjini Nzega, Bashe aliomba pesa kwa ajili kuvuta maji ya ziwa Victoria, na habari njema ni kwamba tayari Mh. Bashe ameshapatiwa Tsh. 200 milioni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu pamoja na kukamilisha ujenzi wa chujio.
Mradi wa maji ya ziwa Victoria utaanza rasmi mwezi februari mwaka ujao (2017).
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment