Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu
Dar Es SalaamNaibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na mbunge wa jimbo la Nzega vijijini, Mheshimiwa Dr. Hamis Kigwangalla, akiwa na kikosi cha wataalam na wana usalama kutoka serikalini, amekamata shehena kubwa ya bidhaa feki na haramu kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar Es Salaam.
Dr. kigwangalla, akiwa na kikosi chake pia wamefanikiwa kukifuma kiwanda bubu kinachotengeneza Konyagi na Smirnoff feki maeneo ya sinza. Kiwanda hicho kinatengenza vinywaji hivyo kwa kutumia spirit inayochanganywa na gongo. Katika kiwanda hicho pia walifanikiwa kukamata chupa tupu na zilizojazwa vinywaji, vizibo, vifungashio pamoja na vifaa vinavyotumika kiwandani hapo.
Akiongoza msako huo wa bidhaa feki, Dkt. Kigwangala alisema, msako huo unafanywa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA.
"Tunafanya msako huu kwa kushirikiana na kikosi kazi cha Serikali ili kuondoa pombe haramu zinazotengenezwa kiholela na kwa kutozingatia viwango vya ubora kwa maendeleo na Afya ya watanzania" alisema Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa msako huo umebaini kwamba watengenezaji hao wanatumia gongo na spiriti kutengeneza pombe kali kitu ambacho ni hatari kwa afya ya watanzania hususani vijana hali inayoweza kupelekea kupoteza nguvu ya Taifa.
Katika msako huo pia ulifanikiwa kukamata maduka yanayouza pombe hizo maeneo ya Mwenge na Manzese jijini Dar es salaam ikiwa chini ya msambazaji Bw. Yusuf Yusuf Abdul Kalambo mkazi wa Kimara ambaye anatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Polisi inawashikilia watu wawili wanaojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa bidhaa hizo feki.
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment