We Like Sharing

Monday, November 21, 2016

Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar

Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar

Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar

Zanzibar, Tanzania

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa chanzo chetu cha habari kilichopo mjini Unguja, Zanzibar, zinasema ajali kubwa ya moto imetokea maeneo ya Mpendae mjini Unguja.

Chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye nyumba hiyo. Moto huo mkubwa umesababisha kuteketea kwa nyumba na mali zote zilizokuwemo ndani ya nyumba hiyo.

Kikosi cha zimamoto kilichelewa kufika katika eneo la tukio kwa sababu taarifa hazikuwafikia mapema lakini wakishirikiana na wananchi waliokuwepo katika eneo la tukio walijitahidi kujaribu kuzima moto huo japokuwa juhudi zao hazikuweza kuokoa mali zilizokuwemo ndani ya nyumba kwa sababu moto ulikuwa mkali sana.

Habari njema ni kwamba, moto huo haukuweza kuwadhuru watu wanaoishi kwenye nyumba hiyo kwani waliwahi kutoka kabla moto haujawa mkali sana.

Picha ya ramani ya Kisiwa cha Unguja, Zanzibar - Tanzania

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment