We Like Sharing

Thursday, December 31, 2015

Makontena 11,884 na magari 2019 yapitishwa bandarini bila tozo

Makontena 11,884 na magari 2019 yapitishwa bandarini bila tozo

Makontena 11,884 na magari 2019 yapitishwa bandarini bila tozo

Dar Es Salaam

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari.

Imebainika kuwa, tarehe 29 December, 2015 makontena 11,884 na magari yapatayo 2019 yenye thamani ya Tsh.48 bilioni yamepitishwa kwenye bandari kavu bila kulipiwa tozo za bandari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusu ufisadi huo ni kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watumishi 15 wa bandari.

Profesa Mbarawa alisema hayo yamebainika baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kufanya ukaguzi katika ICD na CFS zote na hivyo kubaini upotevu huo wa Sh48 bilioni za mapato ya Bandari.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa bandari, Profesa Mbarawa alisema watumishi 15 walikamatwa mnamo tarehe 20 desemba na kufikishwa polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali haitamvumilia mfanyakazi yeyote wa TPA awe mkubwa au mdogo ambaye atajihusisha na upotevu wa mapato ya bandari…” Alisema Mbarawa.

Aliwataja watumishi hao kuwa ni pamoja na Nathan Edward, Aron Lusingu, John Elisante, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Happygod Naftah, Adnan Ally, Masoud Seleman, Bonasweet Kimaina, Bernadeta Sangawe na Zainab Bwijo.

Aidha, profesa Mbarawa aliwaonya Mawakala wa Forodha kuwa serikali itawafutia leseni endapo wataendelea kushirikiana na watumishi wa bandari kutoa mizigo bila kutoa tozo za bandari.

Pia aliwataka mawakala wa forodha 280 wanaotuhumiwa kuhusika katika utolewaji wa makontena na magari bila tozo, kupeleka vielelezo vya uthibitisho ndani ya siku 7 kuanzia tarehe 29 disemba na kuonya kuwa watakaoshindwa kufanya hivyo ndani ya muda husika watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufungiwa kufanya biashara na bandari.

Ikumbukwe pia kuwa siku chache baada ya Waziri mkuu, Kassim Majaaliwa kuapishwa, alifanya ziara ya kushtukiza bandarini ambapo aliibua madudu ya aina hii na ilibainika makontena mengi yalikuwa yamepitishwa bila kulipiwa ushuru, hivyo kulisababishia taifa upotevu wa mabilioni ya fedha.

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

1 comment:

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/serikali-kuanzishwa-wakala-wa-uvuvi-tanzania-kwa-mwaka-2020.1647202/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-nyimbo-tuwapongeze-wasanii-hawa-kupelekea-utamu-wa-siasa-2020.1652542/

    https://www.jamiiforums.com/threads/wizara-ya-viwanda-na-biashara-ipo-kwenye-mchakato-wa-kuanzisha-wakala-wa-shopping-malls-tanzania.1647285/

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kimataifa-vipaumbele-vya-kujenga-reli-na-fursa-za-kibiashara.1647668/767 494826

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kwenye-mzishi-na-ukweli-kuwa-marehemu-alikuwa-anafanya-kazi-sana-na-pengo-lake-haliwezi-zibika.1652710/

    ReplyDelete