Uchafu wa miji nchini Tanzania ni tishio kwa afya za wananchi wanaoishi katika miji hiyo
Tarehe 9 Disemba kila mwaka, Tanzania huadhimisha siku ya uhuru wa Tanganyika ambapo sherehe za maadhimisho hayo kwa kawaida huenda sambamba na Gwaride la kijeshi.
Tofauti na ilivyozoeleka katika miaka yote ya nyuma, mwaka huu siku hiyo ilisherehekewa na wananchi, mashirika mbalimbali na viongozi wa serikali kwa kushiriki kufanya usafi kote nchini kufuatia agizo la Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kuitumia siku hiyo kufanya usafi kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini.
Mwitikio ulikuwa mkubwa kuanzia kwa wananchi, Taasisi zisizo za kiserikali, mashirika binafsi pamoja na watumishi na viongozi wa Serikali akiwemo Rais mwenyewe, Dr. Magufuli ambapo walishiriki kikamilifu katika zoezi hilo la usafi.
Kwa upande wake, Rais alishiriki katika zoezi hilo la usafi katika maeneo yanayozunguka ikulu jijini Dar Es Salaam hadi Ferry, na kueleza kuwa ni aibu kwa taifa kukumbwa na kipindupindu kwa sababu ya uchafu.
Aidha, Rais John Magufuli alisisitiza kuwa zoezi la usafi liwe endelevu na kwamba kila raia ana wajibu wa kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika kudumisha usafi wa maeneo anayoishi ili kukomesha ugonjwa hatarishi wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine yanayoweza kusababishwa na uchafu.
Pamoja na rais kuhimiza suala la usafi, imeonekana kana kwamba suala hilo limepuuzwa kwani maeneo mengi yanaonekana kukithiri kwa uchafu nchini hususani maeneo ya mijini, ambapo ukitembea mitaani utajionea taka nyingi zinazozagaa ovyo.
Hali ni mbaya zaidi kwa maeneo yanayojulikana kwa jina la uswahilini, ambapo taka ngumu kama vile ‘pampas’, na karatasi zilizotapakaa ovyo pamoja na maji taka yenye harufu mbaya ndio ‘habari ya mjini’ kama wasemavyo vijana.
Maeneo mengine ambayo yameonekana kuwa machafu ni masoko makuu ya vyakula, matunda na mboga mboga katika miji mbalimbali nchini hususani majira ya masika ambapo mvua zinaponyesha hupelekea masoko hayo kujaa matope na kutoa harufu mbaya, sambamba na kujaa kwa nzi, wadudu ambao ni hatari sana kwa afya zetu.
Pia baadhi ya masoko/maeneo wanakopikia na kuuza vyakula mama n’tilie yanatisha kiafya, kwa sababu wengi wa mama n’tilie hao hawajali umuhimu wa afya za walaji/wateja wao, wanachojali zaidi ni maslahi au biashara zao tu.
Serikali imejaribu kuwaasa mama n’tilie mara kwa mara kuwa wazingatie suala la usafi katika maeneo wanakofanyia biashara zao, lakini wengi wao hawatekelezi agizo hilo, kitu kinachopelekea kulipuka kwa magonjwa yatokanayo na uchafu hususani kipindu pindu.
Kwa upande mwingine serikali inastahili kulaumiwa kwa kushindwa kuboresha miundombinu ya kusafirishia majitaka. Si ajabu kukuta majitaka yametuama katikati ya njia za watu kwenye makazi yao, mbaya zaidi maji hayo yanatoka vyooni au bafuni. Mvua zinaponyesha, majitaka huchanganyikana na maji ya mvua na kujaa kwenye makazi ya watu kwa kukosa miundombinu ya kuyasafirishia.
Si ajabu pia kukuta jaa la taka likiwa ndani ya makazi ya watu, kitu kinachopelekea taka kusombwa na maji ya mvua hadi majumbani mwa watu, hali ambayo ni hatarishi kwa afya za wakazi wa maeneo hayo.
Ushauri kwa serikali
Serikali ndio mhimili wa taifa na ndio yenye kuamua ni namna gani kero ya uchafu inaweza kutatuliwa. Kuna mamlaka za serikali kama vile manispaa na halmashauri za miji zinazosimamia shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafi, kwa hiyo kuna umuhimu wa halmashauri hizo kusimamia kwa nguvu zote suala la usafi ili kuepusha madhara yasababishwayo na uchafu.Siku ya uhuru mwaka huu Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Naibu waziri wa Afya (wa sasa), Dkt. Hamis Kigwangalla aliandika kwenye wall yake ya Facebook kuwa suala la usafi lifanyike kitaifa kila jumamosi ya mwisho ya kila mwezi. Ni jambo la kheri, ila tatizo ni utekelezaji. Tuna imani serikali ikitumia busara na mamlaka iliyo nayo chini ya Dkt Magufuli, miji yetu bila uchafu itawezekana.
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
https://www.jamiiforums.com/threads/serikali-kuanzishwa-wakala-wa-uvuvi-tanzania-kwa-mwaka-2020.1647202/
ReplyDeletehttps://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-nyimbo-tuwapongeze-wasanii-hawa-kupelekea-utamu-wa-siasa-2020.1652542/
https://www.jamiiforums.com/threads/wizara-ya-viwanda-na-biashara-ipo-kwenye-mchakato-wa-kuanzisha-wakala-wa-shopping-malls-tanzania.1647285/
https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/
https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kimataifa-vipaumbele-vya-kujenga-reli-na-fursa-za-kibiashara.1647668/767 494826
https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/
https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kwenye-mzishi-na-ukweli-kuwa-marehemu-alikuwa-anafanya-kazi-sana-na-pengo-lake-haliwezi-zibika.1652710/