Diamond Platnumz, msanii wa kimataifa kutoka Tanzania
Unaweza kumwita Diamond Platnumz, Dangote au Rais wa Wasafi na majina mengine kibao yanayomtambulisha nyota wa muziki wa Bongo Flavour, Naseed Abdul almaarufu Diamond Platnumz.
Huyu ni miongoni mwa wasanii wa Muziki nchini aliyeitangaza na bado anaendelea kuitangaza Tanzania kupitia Muziki wa Bongo fleva. Amejijengea umaarufu siyo tu hapa nchini, bali pia hadi nchi za nje anajulikana kutokana na jitihada zake za kutoa nyimbo ambazo zimeonekana kuwabamba zaidi wapenzi wa muziki hapa Tanzania na duniani kote kwa ujumla.
Historia yake ya maisha ni ndefu na inatia uchungu na huruma, ila kwa kifupi tu ni kwamba hadi kufikia hatua aliyopo kwa sasa, amepitia changamoto na vikwazo vingi sana kimuziki na hata katika maisha ya kawaida. Ikumbukwe pia kwamba familia ya Diamond haikuwa na uwezo mkubwa sana kiuchumi, jambo lililopelekea Diamond kusoma kwa shida, ila kwa kiasi alichowajalia Mwenyezi Mungu, Diamond aliweza kusoma na kuhitimu elimu ya A-Level.
Kutoka ‘Kamwambie’ hadi ‘Utanipenda’ na kutoka hali ya ufukara hadi umilionea ni hatua ndefu na ya kujivunia kwa kijana huyu. Inasemekana kuwa Diamond Platnumz, ni msanii wa kwanza Tanzania kulipwa pesa ndefu zaidi kupitia harakati zake za kisanaa.
Diamond Platnumz ni msanii pekee Tanzania anayejaza watu wengi kwenye shoo zake ndani na nje ya nchi, kuuza nyimbo zake kwenye kampuni za simu za mikononi ili zitumike kama Ring Back Tones (RBT) pamoja na kupata mialiko yenye malipo makubwa kwenye kampeni za kisiasa na za kibiashara. Vilevile amefanikiwa kusaini mikataba mikubwa yenye pesa ndefu, jambo linalomfanya kuwa tajiri.
Remix ya ‘Number One’ aliyomshirikisha Davido wa Nigeria pamoja na wimbo wa ‘Bambam’ aliomshirikisha Iyanya zilizidi kumpandisha Chati Diamond katika anga za kimataifa kwani aliweza kutambulika zaidi kwa wapenzi na mashabiki wa muziki kutoka nchini Nigeria na nchi nyingine za Afrika Magharibi.
Diamond amewahi kunyakua tuzo nyingi sana, ambapo mwaka 2014 alijizolea tuzo tatu ikiwemo ya mwanamziki mgeni mwenye kipawa kikubwa, mwanamziki bora zaidi kwenye mtindo wa Afro-Pop pamoja na tuzo ya mwanamziki bora zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Pia ndani ya mwaka huo huo, 2014 Diamond aliweza kunyakua tuzo saba katika shindano lililohusisha wanamuziki mbalimbali ambapo miongoni mwa tuzo alizochukua ni pamoja na tuzo ya Mwanamziki bora zaidi wa kiume, Mwaandishi na mtunzi bora zaidi wa nyimbo pamoja na mtumbuizaji bora zaidi Tanzania.
Mwaka huu pia Diamond ameweza kunyakua tuzo kadhaa kama vile Tuzo za AFRIMMA ambapo alinyakua tuzo za Best Male East Africa, AFRIMMA Video of The Year (nyimbo ya ‘Nana’), na Artist of The Year. Hizi ni baadhi tu ya tuzo alizoweza kunyakua Diamond Platnumz katika harakati zake za kisanaa.
Kwa upande wa hapa Bongo, Diamond ni habari ya mjini kiasi kwamba hadi watoto wadogo wanamjua kutokana na nyimbo zake nyingi kuchezwa sana majumbani pamoja na kwenye vituo vya redio na TV. Si ajabu kukuta kijana mtaani kwake anafahamika zaidi kwa majina ya Dangote, Diamond Platnumz, Rais wa Wasafi au Baba Tiffah.
Baadhi ya nyimbo za Diamond zilizompa umaarufu ndani na nje ya Tanzania ni pamoja na Kamwambie, Mawazo, Lala salama, Moyo wangu, Nataka kulewa, Muziki gani pamoja na Number One. Nyimbo nyingine ni pamoja na Number One (Remix), Bam Bam, Mdogo Mdogo, Ninakupenda, Nana na Utanipenda.
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment