Mwenyekiti wa Mtaa Gongo la Mboto akamatwa kwa kosa la kughushi stakabadhi
Dar Es Salaam, TanzaniaMwenyekiti wa mtaa wa Gongo la mboto, Bw. Bakari Shingo, jana alijikuta akiangukia mikononi mwa Polisi baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Maonda kuliagiza jeshi la polisi limkamate mwenyekiti huyo kwa kosa la kukusanya mapato kwa kutumia stakabadhi anazozichapisha mwenyewe kitendo ambacho kinakiuka taratibu zilizowekwa na Halmashauri.
Amri hiyo aliitoa mkuu huyo wa mkoa alipowatembelea wakazi wa Gongo la Mboto katika ziara yake ya siku kumi ya kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wakazi wa Dar Es Salaam, ambapo wananchi walilalamikia uongozi mbaya wa kiongozi huyo ambaye amekuwa akikusanya mapato kwa kutumia stakabadhi za kughushi pamoja na kukaa muda mrefu bila kusoma mapato ya mtaa huo.
Tuhuma nyingine zilizomwangukia Bw. Bakari Shingo, ni kutokuitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu katika mtaa wake, hali inayopelekea wananchi kushindwa kujua namna serikali ya mtaa wao inavyosimamia shughuli za kimaendeleo mtaani hapo.
Tuhuma hizo zilimfanya RC Makonda kuchukua hatua ya kuliagiza jeshi la polisi kuweka rumande mwenyekiti huyo, wakati upeleleziukiendelea kufanyika.
Ziara hiyo ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam ya kulizungukia jiji zima bado inaendelea, ambapo katika ziara hiyo, mkuu huyo wa mkoa amelenga kusikiliza kero zinazowakabili wananchi waishio jijini humo sambamba na kuzipatia ufumbuzi.
Habari zinazofanana na hii
Ziara ya RC Paul Makonda jijini Dar yaibua makubwa
Habari nyingine zaidi...
Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar
Taarifa aliyoitoa Moses Joseph Machali kuhusu kuhamia Chama Cha Mapinduzi
Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi
Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Sikiliza ngoma kali za Mangwea
Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa
Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment