We Like Sharing

Thursday, November 24, 2016

Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe

Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe

Mjue Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Mohamed Bashe

Nzega, Tabora

Mbunge wa sasa wa Jimbo la Nzega Mjini, Bw. Hussein Mohamed Bashe (CCM), alizaliwa mnamo tarehe 26 mwezi wa 8, 1975 katika wilaya ya Nzega, mkoani Tabora. Mheshimiwa Bashe ana mke wa ndoa na wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kike.

Maisha yake ya kielimu

Bwana Mohamed Bashe alianza shule mnamo mwaka 1984, katika shule ya Msingi Kitongo iliyopo katikati ya mji wa Nzega na alihitimu masomo ya elimu ya msingi mwaka 1990.

Mwaka 1994, mheshimiwa Bashe alihitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Badri iliyo mjini Nzega alijiunga na Shule ya Ununio High School iliyopo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kidato cha 5 na 6 ambapo mwaka 1998 alihitimu kidato cha sita. Mheshimiwa Bashe alitunukiwa cheti chake cha Shahada ya Biashara mnamo mwaka 2002 katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Maisha yake ya kikazi

Mheshimiwa Bashe amewahi kushikilia nafasi za uongozi katika mashirika/kampuni mbalimbali. Bashe ni Mkurugenzi Mkuu wa New Habari (2006), Kampuni inayomiliki Magazeti ya Bingwa, Dimba, The African, RAI pamoja na Mtanzania, cheo alichokipata mwaka 2010 na hadi sasa bado anakishikilia.

Bwana Bashe aliwahi kuwa Meneja Mauzo na Usambazaji katika kampuni ya New Habari (2006), kuanzia 2007 hadi 2010 na aliwahi kuwa Meneja Mauzo kuanzia Aprili 2007 hadi Oktoba 2007.

Pia, Bashe amewahi kufanyakazi katika kampuni ya Mwananchi Communications Limited, kampuni inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Magazeti yaliyojizolea umaarufu (The Citizen, Mwanaspoti pamoja na Mwannchi) kuanzia 2006 hadi 2007.

Mheshimiwa Bashe amewahi pia kufanya kazi katika Benki ya NMB kama ofisa wa benki jijini Dar Es Salaam, kuanzia 2003 hadi 2004. Kati ya mwaka 2004 hadi 2005, Bw. Bashe alifanyakazi katika Kampuni ya Celtel Tanzania ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Airtel akiwa Meneja Mauzo.

Maisha yake ya Kisiasa

Mheshimiwa Mohamed Bashe, akiwa ni kiongozi mwenye kipawa cha uongozi, alijaribu kutupa karata yake ya kukigombania kiti cha ubunge kwa mara ya kwanza katika Jimbo la Nzega katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, bahati mbaya hakuweza kupita katika uchaguzi wa ndani ya CCM hivyo hakufanikiwa kugombea.

Katika uchaguazi mkuu wa mwaka 2010, alifanikiwa kushika namba kati ya wagombea watatu, lakini aliwekewa pingamizi kwa madai kuwa yeye sio raia wa Tanzania, hivyo nafasi hiyo ilichukuliwa na Dr. Hamis Kigwangalla ambaye alishikilia jimbo la Nzega kuanzia 2010 hadi 2015.

Mwaka 2015 jimbo la Nzega liligawanya yakapatikana majimbo mawili (Nzega mjini na Nzega Mjini). Mheshimiwa Bashe aligombea jimbo la Nzega Mjini na Mheshimiwa Dr. Kigwangalla aligombea Nzega vijijini wote kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na bahati nzuri wote walifanikiwa kuuchukua ushindi kwa kura nyingi. Takrabani wapiga kura 18,774 walimchagua Bashe ambao ni sawa na 65% ya wapiga kura wote waliojitokeza kupiga kura siku ya upigaji kura.

Tangu aingie madarakani, Mbunge huyo ameshaanza kuzifanyia kazi ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015, ikiwemo ile ya kuwapatia maji wapiga kura wake na alianza kwa kukarabati miundo mbinu ya inayosambaza maji mjini hapo kutoka chanzo cha maji cha bwawa la Kage lililopo maeneo ya Uchama, kaskazini mwa mji wa Nzega.

Ukarabati wa miondo mbinu hiyo umesaidia kupunguza kwa asilimia fulani uhaba wa maji mjini Nzega, na wananchi wamefurahishwa na jitihada hizo za Mheshimiwa Mbunge.

Mbali na ukarabati huo, Mbunge huyo pia kwa jitihada zake amefanikiwa kuishawishi serikali kuu kutoa fedha kwa ajili ya kuanzisha mradi wa kuleta maji ya ziwa Victoria yatakayonufaisha watu wengi zaidi jimboni hapo. Mbali na swala la maji, Bashe pia ametengeneza mazingira ya kuwa karibu sana na wananchi wake, kwa ajili ya kuwawezesha kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwakopesha fedha taslimu kwa ajili ya kuendesha biashara zao, pamoja na kutengeneza fursa mbalimbali zenye mlengo wa kuwanufaisha wananchi kiuchumi.

Mfano mzuri wa uwezeshaji alioufanya Bashe ni ule wa kukopesha pikipiki kwa vijana kwa ajili ya kufanya biashara ya bodaboda, na kuhamisha umiliki wa machimbo ya madini ya Dhahabu katika kitalu cha Namba saba kutoka kwa muwekezaji na kuwapatia wananchi wake. Pia Mheshimiwa amekuwa akitoa mikopo mbalimbali kwa vikundi vya akina mama wajasiriamali jimboni mwake, mikopo ambayo imesaidia vikundi hivyo kujiimarisha katika biashara zao.

Aidha, Bashe pia amewashawishi Airtel kuanzisha huduma ya Airtel Fursa mjini Nzega, huduma ambayo itawanufaisha wananchi kwa kuwapatia mikopo rahisi itakayosaidia kukuza biashara zao.

Mheshimiwa Bashe anatajwa kuwa kiongozi makini na kijana mwenye muono mkubwa ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi, huku akionekan kuwa miongoni mwa vijana wachache ndani ya chama hicho ambao wana uwezo mkubwa wa kubadili taswira ya chama na kukifanya chama chenye nguvu ya ushawishi na ushindani mbele ya watanzania.

Bashe amekuwa kinara wa kukemea na kukosoa utendaji mbaya wa viongozi ndani ya chama chake cha CCM na nje ya chama na maewahi kusema kuwa tatizo kubwa linalosababisha taifa hili kuangamia ni kuwepo kwa sheria nyingi zinazoruhusu wizi, ukwapuaji na kila aina ya ufisadi ni uwepo wa sheria ambazo zilitungwa makusudi na wanasiasa ili baadae waweze kula kiulaini mali za taifa hili pamoja na fedha za walipa kodi wa nchi hii.

Zinazosomwa zaidi
Mbunge wa Jimbo Nzega mjini, Hussein Mohamed Bashe, wa katikati

Habari nyingine zaidi...

Rais Dkt John P Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii

Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA

Moto wateketeza nyumba na mali Unguja, Zanzibar

Taarifa aliyoitoa Moses Joseph Machali kuhusu kuhamia Chama Cha Mapinduzi

Moses Joseph Machali ahamia rasmi Chama cha Mapinduzi

Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu

Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao

Sikiliza ngoma kali za Mangwea

Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa

Hotuba ya Dkt. Hamisi Kigwangalla, alipopokelewa Jimboni Nzega Baada ya Kutangaza nia Kugombea Urais wa Tanzania

Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016

Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

1 comment:

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/serikali-kuanzishwa-wakala-wa-uvuvi-tanzania-kwa-mwaka-2020.1647202/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-nyimbo-tuwapongeze-wasanii-hawa-kupelekea-utamu-wa-siasa-2020.1652542/

    https://www.jamiiforums.com/threads/wizara-ya-viwanda-na-biashara-ipo-kwenye-mchakato-wa-kuanzisha-wakala-wa-shopping-malls-tanzania.1647285/

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kimataifa-vipaumbele-vya-kujenga-reli-na-fursa-za-kibiashara.1647668/767 494826

    https://www.jamiiforums.com/threads/kutana-na-hela-za-manyoka-ipo-siku-kizazi-cha-ku-plan-kitazaliwa-huwa-hakiangaiki.1644150/

    https://www.jamiiforums.com/threads/siasa-za-kwenye-mzishi-na-ukweli-kuwa-marehemu-alikuwa-anafanya-kazi-sana-na-pengo-lake-haliwezi-zibika.1652710/

    ReplyDelete