Kanuni za kuishi na watu vizuri
Mojawapo ya mambo muhimu katika mafanikio ya aina yoyote maishani ni kupata msaada wa aina Fulani kutoka kwa watu wengine. Mtu hawezi kufanikiwa bila msaada wa watu,kwa maana hakuna mtu anayejua kila kitu/jambo na anayeweza kufanya kila kitu Duniani.
Kwa namna yeyote ile mtu anahitaji msaada wa wengine. Hivyo ili kupata msaada wa wengine ni lazima kujua namna ya kuishi na watu vizuri.Ingawa siyo rahisi kumpendeza kila mtu, lakini watu wengi utaishi nao kwa amani. Zifuatazo ni KANUNI na MBINU mhimu za kuishi na watu vizuri
- Uwe na tabia ya kupenda watu wote kwa moyo wote
- Heshimu kila mtu na kila mtu umwone ni muhimu sana na wa maana
- Usimdharau mtu yeyote kutokana na hali yake, hata akiwa ni masikini, hakuelimika, hana cheo cha juu na kadhalika
- Uwe mtu wa furaha na tabasamu unapokutana na watu
- Uwe mcheshi na mtu ambaye watu wanafurahi kuwa nawe
- Usipende kulaumu watu na kama utalaumu mtu,tumia njia nzuri na ya upole ya kumsaidia na kumjenga
- Usiwe msengenyaji na usimseme mtu vibaya
- Usipende kugombeza na kutukana au kutoa matusi kwa watu
- Shukuru kwa kila jambo jema linapotendeka kwa kusema ahsante
- Usiwe mtu wa kujipendekeza kwa watu au wakubwa
- Usipende mabishano na kama yakitokea, usitake kila mara kushinda
- Uwe mpole na usiwe mkali kwa watu
- Usipende kugombana, kupiga au kupigana na watu
- Uwe mnyenyekevu na usijivune kwa kwa lolote lile,kama kuna jambo zuri kwako acha wengine wakusifu
- Usiwe na kinyongo,fitina na usitunze chuki
- Usilipize kisasi,badala yake tenda wema kwa Yule anayekukosea
- Usiwe unachonganisha watu, ukiambiwa udhaifu wa mtu usiende kumwambia aliyesemwa
- Jipende na kujikubali kama ulivyo kimaumbile na uwezo wako,ndipo na watu nao watakupenda na kukubali kama ulivyo
- Tunza siri zako na za wengine
- Usiwe mwepesi wa hasira
- Kumbuka majina ya watu unaokutana nao
- Usiwe mzungumzaji kupita kiasi,badala yake uwe msikilizaji mzuri
- Usiseme uongo au kuongeza chumvi au kupotosha ukweli
- Zungumza kufuatana na mambo mtu anayoyapenda
- Maliza ugomvi au migogoro na wengine kwa njia ya amani kwa kuzungumza na mhusika
- Jifunze kusamehe makosa ya watu
- Unapofanya makosa,kubali na kuungama na kuomba msamaha
- Heshimu na kuvumilia mawazo na maoni ya wengine ambayo ni tofauti na yako
Habari nyingine zaidi...
Dr. Hamis Kigwangalla akamata shehena kubwa ya viroba vya konyagi na pombe haramu
Maofisa wa mbunge, wataalam wa maji na wenyeviti wa mitaa mjini Nzega wafanya kikao
Sikiliza ngoma kali za Mangwea
Trump azidi kutoa kali za mwaka, akataa mshahara mkubwa
Rais John Pombe Magufuli asaini sheria ya huduma za habari 2016
Mambo usioyajua kuhusu Rais mteule, Donald Trump
Uchafu wa miji nchini Tanzania ni tishio kwa afya za wananchi wanaoishi katika miji hiyo
Makontena 11,884 na magari 2019 yapitishwa bandarini bila tozo
Upanuzi wa barabara ya MwanaKwerekwe hadi Fuoni, Zanzibar
Dr. Shein awaonya watakaothubutu kuvuruga amani visiwani Zanzibar
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment