Yanga yapokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga
Dar Es SalaamJana, Club ya Yanga ilipokea kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya club ya Coastal Union, katika mechi ya marudiano iliyochezwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Ushindi huo wa Coastal Union umepunguza makali ya Yanga, ambayo kwa sasa imeshacheza mechi zake 16 na kujizolea point 39, sawa na Azam FC iliyocheza mechi 15 hadi sasa.
Beki wa zamani wa Simba SC, Miraj Adam ndiye aliyefunga bao la kwanza la Coastal Union kunako dakika ya 27 ya mchezo baada ya kuachia shuti la mpira wa adhabu lililompita kipa wa Yanga, Deo Munishi almaarufu ‘Dida’.
Bao la pili la Coastal Union, lilifungwa katika dakika ya 62 ya mchezo huo na mshambuliaji chipukizi wa Coastal Union, Juma mahadhi baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Hamad Juma, na hivyo kuifanya timu hiyo kuibuka mshindi wa mechi hiyo na kuvunja miiko ya Yanga ya kutokushindwa katika mechi zake zilizopita, katika msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom.
Ushindi huo wa Coastal Union ulikuwa malipizi ya mechi ya kwanza waliyocheza na Yanga, ambapo yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Aidha, Coastal ilipata kadi 2 nyekundu kunako dakika za mwesho wa mchezo, ambapo Daktari wa timu, Said Jelan, huku Kelvin Yondani akipigwa kadi nyekundu pia na refa Shamba kutokana na utovu wa nidhamu.
Licha ya kuwa nafasi ya pili kutoka chini katika ligi hiyo, Coastal Union iliutawala mchezo huo, ikiwabana ipasavyo vijana wa jangwani.
Matokeo ya mechi nyingine za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zilizochezwa jana, tarehe 30, januari ni kama ifuatavyo:
- Simba SC 4-0 African Sports
- JKT Ruvu 0-0 Majimaji
- Mwadui FC 1-0 Toto Africans
- Mtibwa Sugar 1-0 Stand United
Paul Makonda aanza ziara ya siku 10 ndani ya jiji la Dar Es Salaam
November 19, 2016
Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za mashirika ya hifadhi za jamii
November 19, 2016
Dr. Shein azindua wodi ya watoto na wazazi
November 19, 2016
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TRA
November 20, 2016
No comments:
Post a Comment