We Like Sharing

Sunday, January 31, 2016

Simba yaendelea kuonesha ubabe kwa African Sports

Simba yaendelea kuonesha ubabe kwa African Sports

Simba yaendelea kuonesha ubabe kwa African Sports

Dar Es Salaam

Hamisi Kiiza (kulia) na Hajji Ugando (kushoto) wakishangilia jana kwenye Uwanja wa Taifa!
Hamisi Kiiza (kulia) na Hajji Ugando (kushoto) wakishangilia jana kwenye Uwanja wa Taifa!

Timu ya Soka ya Simba Sports Club yenye makao yake makuu jijini Dar Es Salaam, jana ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya klabu ya African Sports ya mkoani Taga.

Ni katika mzunguko wa pili wa Ligi kuu, ambapo timu mbalimbali za Tanzania bara zilishuka dimbani katika viwanja mbalimbali. Timu ya simba ilikuwa mwenyeji katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Taifa jana, tarehe 30 mwezi huu.

Simba ilipachika bao lake la kwanza kunako dakika ya 14 ya mchezo, lililofungwa na mganda, Hamis Kiiza aliyepokea pasi kutoka kwa beki Hassan Kessy. Bao la pili lilifungwa na beki Hassan Kessy katika dakika ya 30 ya mchezo.

Kiiza alifanikiwa tena kwa mara ya pili kuzifumania nyavu za lango la African Sports katika dakika ya 42 ya mchezo, lililofanya wekundu wa msimbazi kuwa na jumla ya mabao 3. Simba ilijipatia bao la nne kunako dakika ya 75 ya mchezo, lililofungwa na Hajji Ugando, hivyo kufanya jumla ya magoli manne ya Simba Sports Club.

Hadi mwisho wa mchezo, simba ilikuwa inaongoza kwa magoli 4-0.

Ushindi huo, unaifanya Simba SC ifikishe pointi 36 baada ya kucheza mechi 16, ikizidiwa pointi tatu tu na vinara, Yanga na Azam FC wenye pointi 39 kila mmoja.

Mechi nyingine za ligi kuu zilizochezwa jana tarehe 30 ni kama ifuatavyo:

Yanga ilikuwa mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani kumenyana na Coastal Union, ambapo ilipokea kichapo cha mabao 2-0. JKT Ruvu ilitoka sare ya kutokufungana dhidi ya Majimaji, Toto Africans ilichezea kichapo cha bao 1 kwa sifuri dhidi ya Mwadui FC ambapo Mtibwa Sugar ilitembeza kichapo cha bao 1 kwa sifuri dhidi ya Stand United.

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment