Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Zanzibar, TanzaniaTimu ya Simba Sports Club, imezidi kusonga mbele katika michuano ya kombe la Mapinduzi 2017, yanayoendelea visiwani Zanzibar, baada ya kushinda mechi mbili mfululizo. Mechi ya kwanza walicheza na Taifa Jang'ombe waliyoichapa mabao 2-1, na mechi ya pili walicheza jana usiku na timu ya KVZ, mchezo uliochezwa kwenye dimba la Amaan mjini Unguja amabpo simba waliibuka washindi baada ya kufanikiwa kupachiba bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao, KVZ.
Simba walifunga bao hilo katika dakika ya 43 kupitia kwa Mzamiru Yassin aliyewatoka mbio mabeki wa Timu ya KVZ na kupiga shuti lililomfanya mlinda mlango wa timu ya KVZ kushindwa kulizuia.
Mchezo huo ulianza saa 2:15 usiku, na timu zote mbili zilijaribu kupigana kwa kila namna kwa ajili ya kunyakua pointi 3 za mchezo. Simba walikosa magoli mengi ya wazi, hali kadhalika KVZ walishindwa kutumia vizuri nafasi walizokuwa wanazipata.
Hadi kipindi cha kwanza kinakwisha, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kila timu ilijaribu kupambana kwa ajili ya kumfunga mwenzake lakini hilo lilishindikana kwa sababu kila timu ilijitahidi kulinda lango lake.
Kabla ya mechi kati ya Simba Sports Club na KVZ, mabingwa watetezi wa kombe hilo, URA (kutoka Uganda), jana walikuwa na mtanange mkali baina yao na Jang'ombe Boys, ambapo vijana wa Jang'ombe waliweza kushinda magoli 2-0 dhidi ya URA. Mechi hiyo ilikuwa ya pili kwa Jang'ombe boys, ambapo Mechi ya kwanza walicheza siku ya ufunguzi wa mashindano hayo baina yao na majirani zao (Taifa Jang'ombe) ambapo walipokea kichapo cha bao 1-0.
Kwa sasa Simba SC wanaongoza katika kundi A wakiwa na jumla ya magoli matatu na pointi 6.
Related Articles
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...
Habari nyingine
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment