We Like Sharing

Thursday, January 5, 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Zanzibar, Tanzania

Timu ya Yanga imezidi kuonesha ubabe wa hali ya juu katika michuano ya kombe la mapinduzi inayoendelea viziwani Zanzibar, baada ya kuicharanga mabao mawili kwa nunge klabu ya Zimamoto ya Zanzibar. Mchezo huo umepigwa jioni ya leo (tarehe 4/1/2017), na yanga waliibuka washindi kwa kujinyakulia pointi zote 3 na magoli 2.

Magoli yote mawili yalifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 11 na ya 21 katika kipindi cha kwanza. Yanga walionekana kuwa tishio katika kipindi chote cha kwanza kutokana na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kunako lango la timu ya Zimamoto, hali iliyowafanya wachezaji wa Zimamoto kuingiwa na hofu na kujikuta wakishindwa kuumiliki vizuri mpira.

Hadi kipenga cha mapumziko kinapulizwa Yanga walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kushambuliana ambapo Zimamoto walizidisha mashambulizi kulielekea lango la timu ya yanga, lakini jitihada zao hazikuzaa matunda kutokana na ukuta wa Yanga kuwa imara zaidi.

Yanga ilipata Penati katika dakika ya 50 ambapo, Msuva alipiga lakini alishindwa kufunga baada ya shuti lake kuokolewa na mlinda mlango wa Zimamoto, Juma Hassan.

Katika mashindano haya ya Mapinduzi Cup umoja wa makocha huwa wanachagua mchezaji bora wa mechi, na katika mchezo wa leo kati ya Yanga na Zimamoto, Msuva alitangazwa kuwa shujaa wa mchezo, hivyo Azam walimzawadia Kreti 4 za kinywaji cha Malta.

Kwa matokeo ya mechi hii, Yanga anaendelea kuongoza katika kundi B, akiwa na point 6 na magoli manane, na mechi zote alizocheza hajaruhusu magoli na anatarajia kuingia tena dimbani tarehe 7 mwezi huu atakapoumana na Azam FC katika uwanja wa Amaan mjini Unguja.

Related Articles

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...

Habari nyingine

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment