We Like Sharing

Friday, January 6, 2017

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

Zanzibar, Tanzania

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, URA almaarufu wakusanya mapato wa Uganda, wameshindwa kunyakua pointi 3 za mchezo wa leo baina yao na wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, katika mechi waliyocheza usiku huu katika dimba la Amaan mjini Unguja, visiwani Zanzibar.

Mabingwa hao wamejikuta wakiambulia matokeo ya suluhu ya kutokufungana kutokana na wachezaji wa timu ya Simba kuwa imara katika safu ya ulinzi, hivyo ilikuwa vigumu kwa URA kutikisa nyavu za lango la simba sc.

Mchezo ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili, kwani wachezaji walicheza kwa kushambuliana na kulinda, na hakuna timu iliyoonekana kumzidi mwenzake nguvu au mbinu za ushambuliaji. Mara kadhaa wekundu wa Msimbazi walikosa magoli ya wazi, ambapo badala ya kufunga, wachezaji walipiga nje ya lango la timu ya URA.

Kwa matokeo hayo URA wameambulia pointi moja, na kuwa na jumla ya pointi 4 na wamebakiwa na mchezo mmoja usoni watakaocheza na Taifa Jang'ombe na wanapaswa kushinda mchezo huo ili wafuzu kwenda nusu fainali.

Mpaka sasa Simba SC imeshacheza mechi 3, ambapo mechi ya kwanza walicheza na Taifa Jang'ombe na walifanikiwa kuondoka na ushindi wa 2-1, mechi ya pili walicheza na KVZ ambapo walipata ushindi wa goli bao 1-0, pamoja na mchezo wa leo waliocheza na URA ya Uganda.

Pamoja na matokeo ya suluhu waliyoyapata leo, wekundu hao wa msimbazi bado wanaongoza katika kundi A na wapo katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali. Wekundu hao wamebakiwa na mechi moja watakayocheza na timu ya Jang'ombe Boys ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan.

Kikosi cha Simba kiliundwa na wachezaji hawa: Peter Manyika, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Shiza Kichuya/Hijja Ugando (aliyeingizwa dk87), Muzamil Yassin, Juma Luizio, Laudit Mavugo/Jamal Mnyate (aliyeingizwa dk80) na Pastory Athanas.

Kikosi cha URA kilundwa na wachezaji hawa: Alionzi Nafian, Kulaba Jimmy, Sekito Sam, Mumaba Allan, Ntambi Julius, Muliky Hudu/Elkanah Nkugwa (aliyeingizwa dk74), Lule Jimmy, Bekota Labama, Kigongo Renald/Makogotya Robert (aliyeingizwa dk54) na Kagimu Shafiq.

Related Articles

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...

Habari nyingine

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment