Kampuni kubwa zinazotengeneza simu za Smartphone
Katika somo liliopita nilitoa ufafanuzi juu ya maana ya simu ya mkononi. Katika chapisho hili kama kinavyojieleza kichwa chake, nitaorodhesha majina ya kampuni kubwa zinazotengeneza simu za smartphone pamoja na kutoa ufafanuzi wa kutosha kwa kila kampuni.
Nakuomba usiondoke kwenye ukurasa huu bila kujifunza chochote. ‘Shuka nami’ chini taratibu na kwa umakini mkubwa, si kwa ajili ya kuzijua tu kampuni, bali pia itakusaidia kununua simu madhubuti zaidi siku za usoni.
Apple
Apple ni kampuni ya kimataifa ya kiteknolojia yenye makao yake makuu Califonia, nchini Marekani, ambayo inajishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya umeme kama vile computer, simu za mikononi, Program za kompyuta pamoja na huduma nyingine za kimitandao.Kampuni hii iliingia rasmi kwemye soko la smartphone mnamo mwaka 2007 ambapo kwa mara ya kwanza ilitambulisha rasmi simu zake za iPhone.
Ikumbukwe pia kuwa Apple Inc. ni kampuni inayosifika zaidi katika ulimwengu wa technolojia kutokana na umahiri wake wa kutengeneza vifaa vyenye mwonekano mzuri zaidi, kwa hiyo simu zake pia zina miundo mizuri sana. Simu za iPhone zinatumia Operating System ijulikanayo kama iOS, inayotengenezwa na kampuni yenyewe. Toleo maarufu la simu za iPhone ni iPhone 7, na iphone iliyotolewa hivi karibuni inaitwa iphone 7 plus.
Simu za iPhone ni ghali zaidi kuliko simu nyingine, ndo maana utakuta watu wanaotumia simu hizo ni wachache sana ukilinganisha na simu zinazotengenezwa na kampuni nyingine. Hii inatokana na umadhubuti na uzuri wa simu hizo hivyo watu wengi hushindwa kumudu bei zake, hivyo kuamua kununua simu za kampuni nyingine, kama vile Tecno, Huawei, n.k.
Samsung
Samsung ni kampuni kubwa duniani inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya umeme, ikiwemo simu za mkononi ikiwa na makao yake makuu katika nchi ya Korea ya Kusini. Kampuni hii inazalisha simu kubwa (smartphones) na ndogo (feature phones) na ni kampuni ya kwanza katika utengenezaji wa simu za smartphones.Simu nzuri za Samsung zilizoko sokoni kwa sasa ni pamoja na Samsung z2, Galaxy J2 Pro, Galaxy J7, Galaxy J5, Galaxy J3, Galaxy S7 edge pamoja na Galaxy S7. Simu nzuri zaidi ni Galaxy S7. Simu za Samsung zinatumia Oprating System ya Android.
Hivi karibuni, kampuni hii ilitoa toleo jipya la Galaxy linalojulikana zaidi kwa jina la Galaxy Note 7. Toleo hilo lilileta tafrani sana sokoni kutokana na kuwa na hitilafu ya kuungua inapopata joto kubwa, hivyo toleo hilo halikuuzika sana.
Lenovo/Motorola
Lenovo ni kampuni ya kiteknolojia inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya umeme, hususan Simu, Kompuyta pamoja na program (software) za aina mbalimbali, yenye makao yake makuu Beijinng, China pamoja na Marekani.Kampuni hii ilianzishwa na wanasayanzi wa Jamhuri ya watu wa China mnamo mwaka 1984, jijini Beijing, kwa lengo la kusambaza vifaa vya computer vilivyokuwa vikizalishwa na kampuni kubwa kama vile HP, n.k. Kampuni hii iliinunua kampuni ya IBM mwaka 2005 inayojishughulisha na utengenezaji wa kompyuta.
Kampuni ya Lenovo iliingia katika uuzaji wa simu za Android mnamo mwaka 2011. Mwaka 2013 Lenovo iliibuka kampuni bora katika utengenezaji wa Kompyuta na mwaka 2014 kampuni hiyo ilifanikiwa kuinunua kampuni ya Motorola.
Majina ya simu za Smartphones zinazotengenezwa na kampuni ya Lenovo ni pamoja na Lenovo Z2 Plus, Lenovo A7700, Lenovo A6600 Plus, Lenovo A6600, Lenovo P2, Lenovo A Plus, Lenovo K6 Note, Lenovo K6 Power, n.k. Smartphone ya Lenovo inayouzwa kwa bei kubwa zaidi ni Lenovo Z2 Plus. Simu za Lenovo zinatumia Oprating System ya Android.
Huawei
Huawei ni kampuni ya kichina inayojishughulisha na uzalishaji wa vifaa vya mawasiliano hususani simu za mkononi. Kampuni hii inazidi kutanua wigo wa biashara zake ambapo kwa sasa imefanikiwa kufungua matawi yake katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani.Kampuni hii inatengeneza simu zenye ukubwa tofauti na bei ya simu hizo ni tofauti pia. Baadhi ya smartphones zinazotengenezwa na Huawei ni pamoja na Huawei Mercury, Huawei Ascend D Quad, Huawe Honor Magic, Huawei P9, Huawei P8, nk. Simu za Huawei zinatumia Oprating System ya Android.
LG
LG ni kampuni kubwa na ya kimataifa inayojishughulisha na utoaji wa vifaa na huduma za mawasiliano yenye makao makuu yake nchini Korea. Kampuni hii inatengeneza simu pamoja na vifaa vingine vya majumbani kama vile Televisheni. Iliingiza smartphone yake ya Android ya kwanza sokoni mnamo mwaka 2009 na ilitoa tablet ya kwanza 2011.Kama zilivyo kampuni nyingine zinazozalisha smartphones, kampuni ya LG pia inasifika kwa utengenezaji wa smartphones nzuri, kuanzia rangi hadi miundo yake. Baadhi ya smartphones za kampuni ya LG ni pamoja na LG V20, LG X Skin, LG X5, LG K7 LTE, LG G4, LG G3, LG Google Nexus 5. LG G2, LG Optimus 4X HD, N.k. Simu za LG zinatumia Oprating System ya Android.
Sony
Sony ni kampuni kubwa ya kiteknolojia yenye inayojishughulisha na utoaji wa huduma na vifaa vya umeme zikiwemo simu za mkononi, pamoja na utoaji wa burudani. Makao makuu ya kampuni hii yapo jijini Tokyo nchini Japan.Mwanzoni kampuni hii ilikuwa inajulikana kwa jina la Sony Ericson. Kampuni hii inatoa simu kubwa na ndogo na bei zake zinatofautiana kutegemeana na ukubwa au uwezo wa simu husika.
Baadhi ya simu za smartphones za Sony ni pamoja na Sony Xperia X Z, Xperia X Dual, Xperia C5 Ultra Dual, Xperia Z3 Compact, Xperia Z3, Xperia Z2, Xperia Z1 Compact, Xperia Z1, Xperia Z Ultra, Xperia Z, Xperia Tipo Dual, pamoja na Xperia Neo V. Simu za Sony zinatumia Oprating System ya Android.
Nokia
Kampuni ya Nokia kwa sasa inamilikiwa na kampuni kubwa ya kiteknolojia ijulikanayo kwa jina la Microsoft Corporation yenye makazi yake makuu nchini Marekani. Smartphone za Nokia zinatumia Operating System ya Windows Phone.Baadhi ya smartphones za Nokia ni pamoja na Nokia Lumia 1520, Nokia Lumia 925, Nokia Lumia720, Nokia Lumia 920 na Nokia Lumia 730.
ZTE
ZTE ni kampuni ya kiteknonolojia inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya umeme zikiwemo simu za mkononi na makao makuu yake yako nchini China. Kirefu cha ZTE ni Zhingxing Equipment Corporation. Kampuni imefanikiwa kutengeneza simu na Tablets nyingi za Android.Miongoni mwa simu za smartphones zinazotengenezwa na kampuni ya ZTE ni pamoja na ZTE Nubia Z11 Mini, ZTE Zmax2, ZTE Blade Qlux 4G, ZTE V5, n.k.
Tecno
Kampuni ya Tecno ni kampuni inayotoa bidhaa na huduma za mawasilinano yenye makao makuu yake nchini Uchina. Kampuni hii imefanikiwa kutanua wigo wa biashara zake kwa kusambaza bidhaa na huduma zake katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni hii imewasogezea huduma na bidhaa waafrika kwa kujenga kiwanda chake nchini Ethiopia kinachotengeneza na kusambaza simu zake katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania na.k.Kampuni hii imeleta mapinduzi makubwa katika matumiazi ya simu za mkononi hususan simu za kisasa (smartphones) ambapo inauza kwa bei nafuu sana, hivyo kufanya watu wengi wamudu kununue na kumiliki simu za kisasa.
Baadhi ya simu za smartphone kutoka kampuni ya Tecno ni pamoja Tecno H6, H5, M3, Y4, C8, N8, Y3+ na w3.
Uzuri wa simu za Tecno ni kwamba zinakaa na umeme kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na simu nyingine. Hata sisi Nzegamedia tunatumia Tecno, kwa sababu inakaa chaji muda mrefu na bei yake ni nafuu zaidi.
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment