Lazimisha simu yako isome 3G tu
Asante sana ndugu msomaji kwa kutembelea ukurasa huu hapa Nzegamedia, Nakuahidi hautaondoka ukiwa mtupu (bila kujifunza kitu chenye tija), hivyo nakusihi tuwe pamoja kutoka mwanzo hili hadi mwisho wa somo.
Katika masomo kadhaa yaliyopita niliandika juu ya maana ya mitandao ya 2G, 3G pamoja na 4G. Natumaini masomo hayo yatatoa majibu sahihi kwa wale waliokuwa hawajafanikiwa kupata fafanuzi sahihi ya teknolojia hizo.
Leo kuna mbinu muhimu nimedhamiria kukufundisha. Mbinu yenyewe ni ya kulazimisha laini yako isome signals za 3G tu badala ya kuhama kutoka 2G, 3G n.k kutegemeana na mazingira. Somo hili litajikita zaidi kwenye simu za smartphone zinazotumia Operating System ya Android.
By default, simu za smartphone zinazosapoti huduma za 2G, 3G, 4G, n.k, huwa katika mpangilio wa ‘automatic’ (auto) kwenye aina ya network, kwa maana kwamba simu husika itaweza kusoma 2G, 3G, 4G, n.k kutegemeana na uwezo au nguvu ya mtandao iliyopo katika eneo ilipo simu husika.
Hii huwa kero wakati mwingine, hususan unapokuwa unafanya kitu muhimu kwenye Internet, na unajikuta kasi ya intaneti ipo chini au imeshuka ghafla kutoka 3G hadi 2G. Kwa hiyo nakushauri uipangilie simu yako iweze kusoma 3G tu ili ufurahie kasi ya 3G muda wote.
Fuata hatua zifuatazo rahisi:
- Hakikisha simu yako umeiwasha
- Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
- Bofya Settings
- Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
- Bofya 3G Services
- Kwenye Enable 3G chagua laini unayotaka ikupatie huduma ya 3G
- Kwenye Network Mode chagua 3G au WCDMA Only kutegemeana na simu yako
- Washa Mobile Data
Angalia aina ya mtandao unaosoma kwa kutupia jicho lako juu mwisho kabisa ya kioo cha simu utaona alama yoyote kati ya H, H+ au 3G. Hapo utakuwa umefanikiwa. Ukiona bado haisomi 3G/H/H+ dondosha comment yako hapo chini ili nikufahamishe kwa vitendo.
NB:
Ukiweka 3G/WCDMA Only kwenye maeneo yenye nguvu ndogo ya mtandao laini yako inaweza kushindwa kusoma kabisa, au inaweza kusoma kwa kusuasua. Ukiona hali hiyo utarudisha kwenye ‘auto’ au 2G only ili laini isome vizuri.
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment