Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Zanzibar, TanzaniaKombe la Mapinduzi lilianzishwa mwaka 2007 visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuenzi mapinduzi yaliyoleta uhuru wa Zanzibar mwaka 1964. Michuano ya kombe hili hufanyika kila mwaka mwezi Januari, na hushirikisha vilabu mbalimbali vinavyofanya vizuri visiwani Zanzibar pamoja na vile vya Tanzania bara.
Leo tumekuletea orodha ya majina ya vilabu vyote vinavyoshiriki michuano ya kombe hilo kwa mwaka huu 2017. Angalia kwenye jedwali lifuatalo.
NO | JINA | MAKAAZI | KUNDI |
1 | Simba SC | Dar Es Salaam | A |
2 | Taifa Jang'ombe | Zanzibar | A |
3 | Jang'ombe Boys | Zanzibar | A |
4 | KVZ | Zanzibar | A |
5 | URA | Uganda | A |
6 | Yanga | Dar Es Salaam | B |
7 | Azam | Dar Es Salaam | B |
8 | Jamhuri | Zanzibar | B |
9 | Zimamoto | Zanzibar | B |
Jumla | Vilabu 9 | Znz-5, Bara-3, UG-1 | A-5 & B-4 |
Related Articles
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...
Habari nyingine
URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup
Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment