Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba
Zanzibar, TanzaniaKlabu ya Azam FC yenye makazi yake jijini Dar Es Salaam, jana ilishindwa kutamba kwenye mechi yake dhidi ya Jamhuri FC ya Pemba katika uwanja wa Amaan, mjini Unguja, ambapo mchezo uliisha bila kufungana.
Mchezo huo ulipigwa usiku saa 2:15, na uliwaacha midomo wazi wafuatiliaji wa michuano hiyo, kwani walikuwa wakiamini kuwa Azam lazima wangeondoka na pointi 3 za mchezo, kutokana na klabu ya Jamhuri kuonekana kibonde baada ya kupokea kichapo cha mabao 6-0 kutoka kwa Dar Young Africans katika mechi iliyopigwa tarehe 2/1/2017.
Kwa matokeo hayo klabu ya Azam FC inashikilia nafasi ya 2 katika kundi B la michuano hiyo, ambapo Yanga wapo nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 6 na mabao 8 waliyoyapata katika mechi mbili walizocheza tangu kuanza kwa michuano hiyo mwaka huu.
Tarehe 7 mwezi huu wa kwanza, Azam watakuwa na kibarua kigumu watakaposhuka katika dimba la Amaan mjini Unguja kuumana na mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga, almaarufu wa kimataifa, ambapo nahodha wa klabu hiyo ya Azam FC, John Bocco, amekiri kuwa mechi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na uimara wa klabu ya Yanga.
"Tunawaheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa. Tunajua nasi ni timu kubwa na bora, itakuwa mechi ngumu sana". Alisema John Bocco. "Lakini tunaiweka kando mechi ya leo na tunaanza maandalizi kwa ajili ya mechi ijayo kujiandaa dhidi ya Yanga". Aliongeza.
Aidha, leo wekundu wa msimbazi, Simba SC, watashuka kwenye Dimba la Amaan, katika mechi inayotarajiwa kuwa ni kali baina yao na wakusanya mapato kutoka Uganda, URA, mchezo utakaopigwa usiku saa 2:15. Simba wanaongoza kundi B kwa pointi 6 na magoli 3, na wamesharuhusu goli moja kutoka kwa timu ya Taifa Jang'ombe (Zanzibar).
Related Articles
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...
Habari nyingine
URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup
Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment