We Like Sharing

Tuesday, January 3, 2017

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Zanzibar, Tanzania

Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar.

Mchezo huo ulianza saa 2:15 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, na mwanzo jamhuri walianza vizuri wakifanya majaribio kadhaa hatari ya kuzifumania nyavu za lango la Yanga, jitihada ambazo hazikuzaa matunda kwani mabeki wa Yanga walikuwa makini katika kuzuia mashambulizi ya wachezaji wa Jamhuri.

Baadaeyanga walianza kuonyesha makali yao, kwa kufanya mashambulizi ya nguvu kunako lango la timu ya Jamhuri, ambapo katika Dakika ya 19 mchezaji wa Yanga, Simon Msuva aliweza kupachika bao la kwanza. Katika dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza cha mchezo Yanga walifanikiwa kupachika bao la pili kupitia kwa mshambuliaji wake Donald Ngoma.

Magoli hayo mawili ya Dar Young Africans, yaliamsha furaha za mashabiki wa Yanga, hivyo walianza kushangilia kwa nguvu, kitendo kilichowafanya wachezaji wa Yanga kucheza vizuri zaidi, hali iliyowafanya wapinzani wao, Jamhuri kuchanganyikiwa na kukosa umakini uwanjani. Kunako Dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, Donald Ngoma alifanikiwa kuzitikisa kwa mara ya pili nyavu za lango la timu ya Jamhuri, na kuifanya Yanga kuwa na jumla ya magoli matatu (3) kwa sifuri.

Simon Msuva alipachika bao la 4 katika daika ya 40 ya kipindi cha kwanza. Hadi kipenga cha mapumziko kinapulizwa na mwamuzi, timu ya Yanga ilikuwa inaongoza mchezo kwa magoli 4-0 dhidi ya wenyeji wao Jamhuri.

Kipindi cha pili cha mchezo huo, Yanga waliendeleza kasi yao ya kupeleka mashambulizi makali katika lango la timu ya Jamhuri, na kasi hiyo iliwapatia Yanga bao la tano katika katika dakika ya 59 likifungwa na Thabani Kamusoko. Mchezaji wa yanga, Juma Mahadhi aliwainua vitini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao la 6 katika daika ya 6 akimalizia mprira alioutema golikipa wa Jamhuri.

Hadi kipenga cha kusitisha mpambano huo kikipulizwa na mwamuzi, Yanga walikuwa na jumla ya magoli 6 dhidi ya timu ya Jamhuri ambayo haikuweza kuliona lango la timu ya wazee wa jangwani, na kwa matokeo hayo timu ya Yanga ipo vizuri katika msimao wa michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi.

Kombe la Mapinduzi lilianzishwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuenzi mapinduzi yaliyofanyika mnamo mwaka 1964, ambayo yalifanikiwa kuondoa utawala wa kikoloni visiwani humo. Michuano ya kombe hilo hufanyika mwanzoni mwa kila mwaka.

Related Articles

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...

Soma taarifa kamili hapa

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment