Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Halotel
Asante sana kwa kutembelea blogu yetu pendwa ya Nzegamedia inayokuletea si tu habari za za matukio mbalimbali, bali pia tunakupatia elimu ya teknolojia bila malipo. Kwa hiyo tunakuomba uzidi kung’ang’ana hapa Nzega Media ili uendelee kuhabarika pamoja na kuelimika bila mailipo yoyote.
Katika somo hili nitakufundisha mbinu za kufanya Handset/Data Configurations kwenye simu yako ya Android inayotumia laini ya Halotel. Mtandao wa Halotel ni mchanga katika soko la huduma za simu za mkononi hapa nchini Tanzania, lakini kwa muda mfupi sana imefanikiwa kuleta mapinduzi makubwa hususan kutokana na huduma yake ya Internet kuwa na kasi kubwa.
Halotel ni kampuni inayoongoza hapa Tanzania kwa kuwa na huduma ya Internet yenye kasi zaidi kuliko mitandao mingine kwa sasa, hivyo kuna haja ya wewe kumiliki laini ya Halotel na kuifanyia Configurations nzuri/sahihi ili ufurahie Internet ya Kasi wanayofurahia wengine.
Fuata hatua zifuatazo ili uweze kufanya settings sahihi za Internet kwa Android inayotumia laini ya Halotel:
- Hakikisha simu yako umeiwasha
- Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
- Bofya Settings
- Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
- Bofya Access Point Names (APN) Kama simu ina inatumia laini mbili (Dual SIM), chagua laini unayotaka kuifanyia configuration kwa kubofya kwenye jina lake
- Bofya kwenye kitufe cha menu ya simu yako kilichopo chini ya kioo cha smartphone yako, au kinaweza kuwa juu kulia mwa kioo cha simu kutegemeana na aina ya simu.
-
Chagua New APN kisha jaza taarifa kwenye visanduku vya maandishi kama nilivyoainisha hapo chini.
Name: HALOTEL
APN: b-internet
APN type: default
Authentification type: PAP, CHAP, PAP or CHAP, None
Ufafanuzi
Kama unavyoona hapo juu maandishi unayoingiza hakikisha yanakaa katika mpangilio huo. Unapotakiwa kuandika herufi ndogo andika herufi ndogo na unapotakiwa kujaza herufi kubwa jaza herufi kubwa kwani kinyume chake simu yako haitaungwa kwenye Internet.Kwenye Name jaza HALOTEL kwa herufi kubwa. Kwenye APN jaza b-internet na herufi zote ziwe ndogo. Kwenye APN type jaza au chagua default kwa herufi ndogo. Kwenye Authentification type chagua yoyote katika listi inayokuja: PAP or CHAP, nk.
Baada ya kujaza taarifa zinazohitajika kwa usahihi, bofya tena kwenye menu ya simu yako Chagua Save
Sasa waweza kuwasha Data uanze kufurahia ulimwengu wa internet kwa kutumia simu yako kupitia laini ya Halotel. Kwa maswali au msaada zaidi unaweza kunipigia simu kupitia 0655251774
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment