Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Zantel
Asante sana ndugu msomaji kwa kuwa pamoja nasi hapa Nzegamedia. Somo la leo kima kinavyojieleza kichwa chake litajikita zaidi katika kuelekeza namna ya kufanya Handset Configurations au APN settings kwa smartphone za Android zinazotumia laini za Zantel.
Hatua za Data Configurations ni rahisi sana, kwa hiyo tunakusihi ushuke hapo chini kwenye hatua zenyewe:
- Hakikisha simu yako umeiwasha
- Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
- Bofya Settings
- Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
- Bofya Access Point Names (APN) Kama simu ina inatumia laini mbili (Dual SIM), chagua laini unayotaka kuifanyia configuration kwa kubofya kwenye jina lake
- Bofya kwenye kitufe cha menu ya simu yako kilichopo chini ya kioo cha smartphone yako, au kinaweza kuwa juu kulia mwa kioo cha simu kutegemeana na aina ya simu.
-
Chagua New APN kisha jaza taarifa kwenye visanduku vya maandishi kama nilivyoainisha hapo chini.
Name: ZANTEL
APN: znet
APN type: default
Authentification type: PAP, CHAP, PAP or CHAP, None
Ufafanuzi
Kama unavyoona hapo juu maandishi unayoingiza hakikisha yanakaa katika mpangilio huo. Unapotakiwa kuandika herufi ndogo andika herufi ndogo na unapotakiwa kujaza herufi kubwa jaza herufi kubwa kwani kinyume chake simu yako haitaungwa kwenye Internet.Kwenye Name jaza ZANTEL kwa herufi kubwa. Kwenye APN jaza znet na herufi zote ziwe ndogo. Kwenye APN type jaza au chagua default kwa herufi ndogo. Kwenye Authentification type chagua yoyote katika listi inayokuja: PAP or CHAP, nk.
Baada ya kujaza taarifa zinazohitajika kwa usahihi, bofya tena kwenye menu ya simu yako Chagua Save
Sasa waweza kuwasha Data uanze kufurahia ulimwengu wa internet kwa kutumia simu yako kupitia laini ya Zantel. Kwa maswali au msaada zaidi unaweza kunipigia simu kupitia 0655251774
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment