4G LTE ni nini?
Maneno haya mawili (4G & LTE) yanatumika pamoja lakini kila moja lina tafsiri tofauti. Tutayafafanua yote kwa ufasaha ili uweze kuyaelewa na yasikupe shida siku nyingine.
4G ni jina linalotumika kuwakilisha kizazi cha nne katika teknolojia ya mitandao ya simu za mkononi. Kirefu cha 4G ni ‘Fourth Generation’. LTE ni kifupi cha’ Long Term Evaluetion’, na ni sehemu ya teknolojia ya 4G.
Huduma ya 4G hutoa intaneti yenye kasi mara tano zaidi ya 3G, hivyo kufanya kasi ya kupakia (upload) na kupakua (download) kuwa kubwa zaidi kuliko 3G.
Umoja wa Mamlaka ya Kimataifa inayosimamia Mawasiliano duniani (ITU) haijatoa maelezo ya kipimo sahihi cha kasi ya 4G, ila kwa kifupi tu ni kwamba huduma hii hubadilika kasi yake kutegemeana na mazingira, miundombinu pamoja na hali ya hewa. Inasemekana kuwa kasi ya kupakua katika mtandao wa 4G inaweza kufikia 100mb kwa sekunde na kasi ya kupakia inakisiwa kuwa 50mb kwa sekunde.
4G hutumia masafa mbalimbali kusafirisha taarifa kutoka kifaa kimoja kwenda kingine kwa kasi kubwa, na ili uweze kutumia huduma hii ni lazima simu au modem yako iwe imewezeshwa kutumia huduma hii.
Ukiwa na mtandao huu wenye kasi kubwa unaweza kufanya mambo mbalimbali kwenye Internet kwa haraka sana kuliko ilivyo kwenye vizazi vilivyotangulia (2G & 3G). Kwa mfano unaweza kupakua viambatanisho vya barua pepe kwa haraka sana, au unaweza kupakua vipande vya video ulivyotumiwa kwenye mtandao wa WhatsApp kwa haraka zaidi. Kwa kifupi kwenye 4G hakuna mwendo wa kinyonga…
Teknolojia ya 4G LTE imeanza zamani katika nchi za wenzetu, lakini nchini mwetu imeanza mwshoni mwa mwaka 2015, na kampuni kongwe nchi, Tigo ndiyo kampuni ya kwanza kuleta huduma hiyo ikifuatiwa na kampuni mingine, kama vile Vodacom, Zantel, Airtel na Halotel. Kwa sasa kampuni zote za simu za mkononi nchini zinatoa huduma hiyo lakini haijatawanya huduma hiyo katika maeneo mengi nchini kwa hiyo wanaotumia huduma hii ni wachache sana.
Huduma ya 4G nchini Tanzania
Huduma ya 4G nchini mwetu, Tanzania inasuasua sana kutokana na sababu mbalimbali. Zipo sababu za kiufundi na zipo sababu za kiuchumi. Miongoni mwa sababu za kiuchumi ni ughali wa bei ya kununua simu zenye uwezo wa kutumia mtandao wa 4G. Bei ya chini ya kununua simu ya 4G ni Tsh.300,000/=, na hali ya uchumi ilivyombaya kwa watanzania wengine inakuwa vigumu mtu kutupa pesa kubwa kiasi hicho.Sababu ya pili ambayo ni ya kiufundi, inazihusu moja kwa moja kampuni za simu za mikononi kwani zimeshindwa kutawanya huduma hiyo katika maeneo mengi nchini, kwa mfano mtandao wa Tigo katika mji wa Zanzibar unatoa huduma ya 4G katika mitaa isiyozidi 6 mjini humo. Pia, pamaoja na kutoa huduma hiyo, wateja wanaotumia huduma ya 4G nchini wanadai kasi ya huduma hiyo haiendani na matangazo ya kampuni zinavyojipamba.
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment