Lazimisha simu yako isome 4G tu
Baada ya kuona watumiaji wengi wa simu za Android wanalalamika kuwa simu zao zina uwezo wa kutumia mtandao wenye kasi zaidi (4G) lakini wakiwasha data simu zao hazisomi 4G na badala yake zinasoma 2G/E au 3G/H/H+, nimeamua kuwaletea mbinu za kutatua changamoto zao.
Yawezekana hata wewe ni miongoni mwao, kwa hiyo nakupongeza kutembelea nzegamedia, maana muda si mrefu utakuwa na ujuzi wa kutatua tatizo hilo.
Somo hili halitaangalia wewe unatumia mtandao gani (Tigo, Voda, n.k), maana ujuzi huu waweza kutumika kwenye mitandao yote duniani.
Kutumia kasi ya 2G au 3G kwenye simu yenye uwezo wa kutumia kasi ya 4G ni kuidhalilisha simu husika, hivyo nakushauri ufuate hatua zifuatazo rahisi zaidi ili ujue namna ya kulazimisha simu yako kusoma 4G tu:
- Hakikisha simu yako umeiwasha
- Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
- Bofya Settings
- Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
- Bofya 4G/LTE Services
- Kwenye Enable 4G chagua laini unayotaka ikupatie huduma ya 3G
- Kwenye Network Mode chagua 4G/LTE Only kutegemeana na simu yako
- Washa Mobile Data
Hapo utakuwa umefanikiwa kulazimisha simu yako kutumia mtandao wa 4G tu. Ukiona bado haisomi 4G/LTE dondosha comment yako hapo chini ili nikufahamishe kwa vitendo.
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment