We Like Sharing

Thursday, January 12, 2017

Jinsi ya kuweka screen lock kwenye simu ya android

Jinsi ya kuweka screen lock kwenye simu ya android

Jinsi ya kuweka screen lock kwenye simu ya android

Kama ulifuatilia vizuri kwenye somo lililopita la screen lock ni nini? naimani una ufahamu mzuri wa nini maana ya screen lock. Kama hufahamu maana ya screen lock, nakushauri ubofye hapa ili upate ufahamu zaidi kabla hatujaendelea na somo letu.

Simu za kisasa, zinafanyakazi kubwa sana, hata zile kazi zinazotakiwa kufanywa na kompyuta, unaweza kuzifanya kwa kutumia simu yako. Kazi hizo ni pamoja na kuchati na marafiki kwenye mitandao ya kijamii, kutuma na kupokea barua pepe, kuhifadhi taarifa binafsi za benki, n.k.

Taarifa unazohifadhi kwenye simu yako ni nyeti sana kuliko vile unavyofikiria, hivyo zinahitaji ulinzi ili zisiangukie kwenye mikono mibaya zikaharibu mfumo mzima wa maisha yako. Ikumbukwe pia sio kila unayecheka nawe ana furaha na wewe kutoka moyoni, wengine wana chuki mioyoni na wanahangaika kwa kila namna kwa ajili ya kukuharibia maisha yako, eidha kwa kukuibia hela kwenye akaunti zako za benki, au kuvujisha taarifa zako nyeti kwa lengo la kukuaibisha.

Njia pekee ya kuepusha kuvuja kwa taarifa zako nyeti, ni kuweka screen lock, huduma ambayo itakuhakikishia ulinzi wa taarifa zilizomo kwenye simu yako na kukufanya kuwa ni mtu pekee mwenye mamlaka ya kuona taarifa zako binafsi.

Bada ya maelezo hayo ya utangulizi, nakuomba sasa tuende moja kwa moja kwenye hatua za kuweka lock kwenye simu yako. Fuata hatua zifuatazo kwa usahihi lakini tunakushauri kuweka vizuri kumbukumbu za passwords, patterns, au PIN zako utakazoweka ili iwe rahisi kuzikumbuka unapofungua simu yako.

  1. Washa simu yako
  2. Bofya menu kuu ya simu
  3. Chagua Settings
  4. Chagua Security
  5. Bofya Screen lock
  6. Chagua aina ya screen lock unayopendelea kama vile slide, voice Unlock, Face Unlock, Patterns, PIN, n.k.
  7. Jaza taarifa zinazohitajika kutegemeana na aina ya screen lock kisha bofya Continue
  8. Rudia kujaza taarifa kisha bofya OK au Confirm
  9. Tayari umeshafanikiwa kuweka screen lock.

Related Articles

Screen lock ni nini?

Kampuni kubwa zinazotengeneza Smartphones

3G ni nini na inafanyaje kazi?

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment