We Like Sharing

Thursday, January 12, 2017

Screen lock ni nini?

Screen lock ni nini?

Screen lock ni nini?

Screen lock ni feature ya kiulinzi inayotumika kwenye kompyuta na simu za mkononi kwa ajili ya kulinda vifaa hivyo pamoja na taarifa zake dhidi ya watu wasio na mamlaka ya kutumia vifaa husika.

Screen lock huhitaji kitendo Fulani kufanyika kwa usahihi ili kumruhusu anayetaka kutumia kifaa kilichowekewa screenlock. Kitendo hicho kinaweza kuwa kuchora kwenye kioo (patterns), kuingiza PIN au Neno la siri kutegemeana na aina ya screen lock iliyowekwa kwenye kifaa husika.

Somo letu la leo litajikita zaidi katika screen lock ya kwenye simu za mkononi. Kwenye simu zetu za mkononi tunahifadhi taarifa za aina mbalimbali ikiwa ni pamoja namba za simu, akaunti za barua pepe au mitandao ya kijamii, video, picha, taarifa za benki, meseji tunazotumiwa na watu wetu wa karibu, n.k.

Taarifa nyingine ni za siri au nyeti sana kiasi kwamba zikiangukia kwenye mikono ya watu wasiohusika au wabaya inaweza kuleta gharama kubwa katika maisha yetu.

Katika pitapita zako unaweza kujikuta umepoteza simu yako, eidha kwa kuisahau mahali, kuibiwa kiujanja au kuporwa. Huwezi kujua atakayeichukua simu yako ataitumia vipi, maana tumeshuhudia kesi nyingi za watu kuibiwa/kupoteza simu zao na kisha wanaoiba simu hizo wanawapigia watu waliopo kwenye phonebooks za simu zilizoibiwa/kuokotwa kwa lengo la kufanya utapeli.

Na ukizingatia siku hizi mitandao ya kijamii inatengenezwa kila kukicha na ile ya zamani inaboreshwa, kitu kinachotufanya tushinde kutwa nzima na usiku kucha mitandao tukichati na marafiki zetu, tukituma taarifa za aina mbalimbali, ambapo nyingine ni nyeti sana. Vipi atakayeokota simu yako akivujisha mawasiliano yako ya siri au ya faragha kwenye WhatsApp, Facebook au Instagram? Utajisikiaje?

Changamoto zote hizo waliziona mapema watengenezaji wa simu za mkononi hivyo wakaweka teknolojia ya kufunga kioo cha simu yako ili watakaofungua simu yako na kukagua madudu ya kwenye simu yako ni wale unaojuana nao tu na sharti uwape ruhusa, kwa maana ya kuwafundisha namna ya kutoa screenlock yako.

Ukiiwekea screen lock simu yako, kila inapolala (sleep), ukiiamsha itakuomba uweke Password, Pattern, PIN, n.k kutegemeana na aina ya screen lock unayotumia kwenye simu yako ili itoe ruhusa kufanya shughuli yoyote, kama vile kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, n.k.

Aina za screen lock zilizomo kwenye simu za Android

Asilimia kubwa ya simu zinazotumia Android Operating System, zina aina zifuatazo za screen lock:

Slide

Slide ni aina ya screen lock inayotumika sana. Mara nyingi ukinunua simu mpya ya smartphone utakuta screen lock yake ni hii ya slide, ama kwa kitaalam wanasema Slide ni default screen lock kwenye simu nyingi za Android. Udhaifu wake ni kwamba haina masharti magumu ya namna ya kuitoa au kufungua simu, kwani mtu akipangusa tu kioo simu hufunguka na kumruhusu mtumiaji kuanza kutumia simu, kwa hiyo haisaidii kulinda taarifa zako za siri.

Aina hii ya lock screen husaidia tu simu yako kutokujiwasha na kuanza kufanya kazi bila wewe mwenyewe kujua. Kwa ulinzi zaidi chagua aina zilizoorodheshwa hapo chini.

Face Unlock

Aina hii ya lock huhitaji mmiliki wa simu kuangalia kioo cha simu baada ya kuiamsha simu yake na sura lazima iwe ndani ya kiumbo cha duara kinachokuwepo kwenye kioo. Mfumo ukigundua kuwa sura sio sahihi simu haiwezi kujifungua, hadi itakapokuja sura iliyotumia ku_set lock hiyo. Aina hii hutumia Face recognition technology, ambapo sura inayofungua simu husika ni ile tu iliyorekodiwa wakati wa ku_set lock.

Pamoja na aina hii kuonekana nzuri kuliko Slide, wataalam wanaeleza kuwa ni rahisi sana kwa wajanja/wadukuzi kufungua simu yako kama utaweka aina hii ya screenlock. Aina zilizoorodheshwa hapo chini zina nguvu zaidi ya kiulinzi wa simu na data zako kuliko hii.

Pattern

Pettern ni aina ya lock screen ambapo mtumiaji anatakiwa apitishe mstari kwenye vyumba vya duara kwa kuchora kwa vidole vyake baada simu kuamshwa. Hii ni miononi mwa njia ambayo inatoa ulinzi na usalama wa kuaminika zaidi kuliko Slide na Face Unlock.

PIN

Neno PIN ni kifupi cha Personal Identification Number. Katika aina hii ya lock mmiliki wa simu anatakiwa kuingiza namba tu kuanzia tarakimu nne na kuendelea. Anaweza kuingiza namba zotote (0, 1-9).

Password

Password ni neno la siri ambalo mtumiaji wa simu anaweka kwenye simu yake kwa ajili ya kufungua simu yake. Password ni tofauti na PIN kwa sababu inaruhusu kuweka mchanganyiko wa herufi na namba.

Related Articles

Jinsi ya kuweka screen lock kwenye android

Kampuni kubwa zinazotengeneza Smartphones

Handset/Internet Configurations za simu za android

Mambo ya kufanya baada ya kununua smartphone

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment