We Like Sharing

Tuesday, January 10, 2017

Jinsi ya kufanya Handset/Internet Configurations kwenye simu za android

Jinsi ya kufanya Handset/Internet Configurations kwenye simu za android

Jinsi ya kufanya Handset/Internet Configurations kwenye simu za android

Katika somo liliopita tulitaja pamoja na kufafanua mambo muhimu ya kufanya mara baada tu ya kununua simu yako ya smartphone. Katika somo la leo tutazungumzia mbinu za kufanya settings za Internet ili simu yako iweze kutumia mobile data, na wewe upate nafasi ya kutumia internet.

Hatua za kufanya Handset Configurations hutofatiana kutegemeana na aina ya simu inayofanyiwa configuration pamoja na mtandao wa simu za mkononi anaotumia mteja husika. Kwa hiyo utambue kitu muhimu kuwa kila mtandao wa simu za mkononi una mipangilio yake binafsi ya Internet inayotofautiana na mitandao mingine, vivyo hivyo hata simu pia zinatofautiana hatua za kufanya internet configurations, kutegemeana na Operating System iliyomo kwenye simu husika au kutegemeana na aina ya simu.

Katika somo hili tutazungumzia namna ya kufanya settings za internet kwa simu za smartphone zinazotumia Android Operating System. Pia tutajikita katika mitandao ya simu za mikononi inayofanyakazi (operating) ndani ya nchi ya Tanzania hususan, Tigo, Airtel, Vodacom, Halotel pamoja na Zantel.

Kuna watu wanafikiri ni vigumu sana kufanya Internet configurations, hadi wanaamua kwenda vibandani kusaidiwa na mawakala wa mitandao au mafundi simu, hivyo hujikuta wakipoteza pesa zao kwa kazi ndogo ambayo hata wao wanaweza kukifanya na wakasevu pesa zao kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Hatua za configurations ni chache na ni rahisi sana hususan kama wewe ni mtundu au mzoefu wa kuchezea au kutumia simu za mkononi. Changamoto ni kwa wale wenye uzoefu mdogo wa kuchezea simu, lakini niwatoe wasiwasi kwa sababu Nzegamedia huwa tunafafanua vizuri sana kiasi kwamba ni rahisi kwa mtu yeyote kuelewa somo.

Kwa kuwa kila mtandao wa simu za mkononi una hatua ndefu za kufanya Handset configurations, tumeligawa somo letu hili katika makundi matano kulingana na idadi ya mitandao tutakayoigusia. Kwa hiyo nakuomba ubofye kiungo (link) hapo chini kwa kuchagua mtandao wako unaopenda kujua namna ya kuufanyia data configurations.

Kwa Internet configurations za laini ya mtandao wa Tigo bofya hapa
Kwa Internet configurations za laini ya mtandao wa Vodacom bofya hapa
Kwa Internet configurations za laini ya mtandao wa Airtel bofya hapa
Kwa Internet configurations za laini ya mtandao wa Halotel bofya hapa
Kwa Internet configurations za laini ya mtandao wa Zantel bofya hapa

Tunakutakia usomaji mwema, na usisahau kutoa maoni yako pamoja na kusambaza somo hili kwa watu wako wa nguvu. Kwa maswali yoyote yanayohusiana na somo hili, au mengine waweza kumtumia kiongozi mkuu wa Nzegamedia kupitia 0655251774.

Related Articles

Internet Configurations za Halotel

Internet Configurations za Zantel

Internet Configurations za Airtel

Internet Configurations za Vodacom

Kampuni kubwa zinazotengeneza Smartphones

Internet Configurations za Tigo

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment