We Like Sharing

Tuesday, January 10, 2017

Simba SC na Yanga kukutana uso kwa uso Kombe la Mapinduzi

Simba SC na Yanga kukutana uso kwa uso Kombe la Mapinduzi

Simba SC na Yanga kukutana uso kwa uso Kombe la Mapinduzi

Zanzibar, Tanzania

Kesho itakuwa siku muhimu sana kwa wapenzi wa soka visiwani Zanzibar na Tanzania bara hususan mashambiki wa vilabu vya Simba na Yanga, kutokana na watani wajadi hao kuwa na mchezo mkali na wa kusisimua katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar majira ya saa 2:15 usiku.

Mchezo huo ni wa nusu fainali katika mashindano ya kombe la mapinduzi, ambapo Simba SC wamefuzu kuingia nusu fainali wakiwa na jumla ya pointi 10 katika kundi A, wakifuatiwa na timu ya Taifa Jang'ombe waliochuma pointi 6 katika mzunguko wa kwanza wa mashindano hayo.

Kwa wa watoto wa Jangwani, Dar Young Africans, wapo katika nafasi ya 2 ya kundi B wakiwa na jumla ya pointi 6, kwa hiyo wanaongozwa na wana lamba lamba (Azam) wenye jumla ya pointi 7.

Kwa mujibu wa utaratibu wa mashindano haya, Yanga, waliokamata nafasi ya 2 kundi B, watakutana na wekundu wa msimbazi, Simba SC waliopo nafasi ya 1 katika kundi A, ambao hawakupoteza hata mchezo mmoja katika mzunguko wa kwanza wa mashindano hayo.

Yanga wanakwenda nusu fainali wakiwa na maumivu mioyoni, kutokana na kichapo cha mabao 4-0 walichopewa na wana lambalamba, kwani hawakutegemea kabisa kufungwa magoli mengi kiasi hicho na Azam, kwani Azam walianza mashindano kwa kucheza michezo isiyo na mashambulizi hatarishi kwa timu pinzani.

Pamoja na kichapo hicho, Yanga wanapaswa kutulia na kucheza kwa kujiamini zaidi na kufanya mashambulizi kuelekea kwa wapinzani wao, ili waweze kujipatia pointi nzuri zitakazowapeleka fainali pamoja na kuwafurahisha mashabiki wao, ambao tangu wapokee kipigo kutoka kwa wanalambalamba, nyuso zao zinaonekana kujawa na aibu.

Halikadhalika, wekundu wa msimbazi nao wanatakiwa kupata ushindi katika mechi ya kesho ili wajiweke katika nafasi nzuri itakayowapeleka fainali pamoja na kuwafurahisha mashabiki wao.

Kwa kifupi mchezo wa kesho utakuwa na ushindani mkubwa sana kwa timu zote mbili, hususan kutokana na mashabiki wa timu zote mbili kutambiana na kuonyeshana majigambo ya hali ya juu, kila mmoja akidai kuwa timu yake ndiyo itaondoka na ushindi kesho.

Related Articles

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...

Habari nyingine

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment