We Like Sharing

Monday, January 9, 2017

Simba yaifunga Jang'ombe Boys 2-0 Kombe la Mapinduzi

Simba yaifunga Jang'ombe Boys 2-0 Kombe la Mapinduzi

Simba yaifunga Jang'ombe Boys 2-0 Kombe la Mapinduzi

Zanzibar, Tanzania

Wekundu wa msimbazi, Simba SC, wameendeleza wimbi la kutoa kichapo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa 2-0 timu ya Jang'ombe boys katika mechi kali iliyochezwa leo (8/1/2017) jioni.

Timu zote ziliingia uwanjani zikiwania nafasi ya kufuzu kuingia nusu fainali, ambapo wekundu wa msimbazi walikuwa wanahitaji eidha suluhu au ushindi katika mechi hiyo ili watinge nusu fainali, lakini bahati nzuri wamefanikiwa kupata mabao 2-0 na kupata jumla ya pointi 10.

Mabao yote Yametiwa nyavuni na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Burundi, Laudit Mavugo. Bao la kwanza alifunga dakika ya 11 katika kipindi cha kwanza, kwa kuupiga mpira uliokuwa umerudi baada ya kugonga nguzo za goli, kutokana na shuti kali iliyopigwa na kichuya.

Bao la pili alifanikiwa kufunga katika kipindi cha pili baada ya kupokea tena pasi kutoka kwa Kichuya, ambapo alijivuta hadi ndani ya himaya ya 18 na kuachia shuti kali ililyomshinda kuizuia mlinda mlango wa Jang'ombe Boys.

Baada ya bao la pili, jang'ombe waliingiwa na hofu hivyo wakajikuta wakishindwa kuumiliki vizuri mpira, kitendo kilichowapa nafasi zaidi wapinzani wao, Simba kutawala mchezo na kufanya mashambulizi hatari ya mara kwa mara kuelekea langoni mwa timu ya vijana hao wa Jang;ombe.

Kwa upande mwingine, Mavugo ameibuka kinara wa mchezo wa leo, na amepatiwa zawadi na Kampuni ya Azam, ambao ndio wadhamini wa kombe hilo mwaka huu.

Kwa matokeo hayo simba wanaendelea kuongoza kundi B wakiwa na jumla ya pointi 10, hivyo wamefuzu kuelekea nusu fainali, ambapo, ambapo watakutana na watani wao, Dar Young Africans (Yanga) jumanne ya wiki inayoanza kesho, mchezo ambao utapigwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Related Articles

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...

Habari nyingine

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment