Yanga yapigwa 4 bila na Azam FC Kombe la Mapinduzi
Zanzibar, TanzaniaClub ya Dar Young Africans almaarufu wa kimataifa kutoka mitaa ya Jangwani jijini Dar Es Salaam, jana walipokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa 'Wanalambalamba' (Azam FC), katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Amaan mjini Unguja Zanzibar, katika michuano ya kuenzi mapinduzi ya Zanzibar iliyopewa jina la Mapinduzi Cup au Kombe la Mapinduzi
Mchezo ulianza kwa kasi sana, na dakika 1 ya kwanza ya mchezo timu zote zilionekana kushambuliana kwa zamu. Kunako dakika ya 2 kipindi cha kwanza cha mchezo, Azam walifanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa nahodha wa klabu hiyo, John Raphael Bocco aliyemalizia mpira uliokuwa unatembea baada ya kupanguliwa na mlinda mlango wa timu ya Yanga, Deogratius Munishi, almaarufu Dida.
Kabla ya mchezo huo Yanga walikuwa wanaongoza kundi B wakiwa na jumla ya pointi 6 na magoli 8, lakini baada ya mchezo huo Azam ilipanda kileleni na kumfanya Yanga ashuke hadi nafasi ya Pili katika kundi B.
Baada ya bao hilo Yanga walijaribu kufanya mashambulio kadha langoni mwa timu ya Azam lakini majaribio yao hayakuzaa matunda kutokana na safu ya ulinzi ya Azam kuwa imara zaidi.
Azam walikuwa hawawapi Yanga nafasi ya kukaa na mpira kwa muda mrefu, walikuwa wanawavizia na kuwapokonya mpira waachezaji wa Yanga. Hadi kipenga cha mapumziko kinapulizwa, Azam walikuwa mbele ya yanga kwa bao 1-0.
Katika kipindi cha pili, Azam hawakuwapa Yanga nafasi ya kupumua, bali waliendeleza kasi yao ya kufanya mashambulizi kuelekea katika lango la timu ya Yanga. Azam walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa mshambuliaji, Mghana, Yahya Mohammed aliyepiga kwa kichwa mpira uliopigwa na Sure Boy.
Azam waliendeleza mashambulizi, na katika dakika ya 80 ya mchezo, walifanikiwa kuzitikisa nyavu za timu ya Yanga kwa mara ya tatu, baada ya Mahundi kupiga shuti ndefu iliyompita mlinda mlango wa Yanga.
Bao la 4 lilifungwa na Winga Mghana, Enock Atta Agyei, kunako dakika ya 85 ya mchezo, baada ya kupokea pasi kutoka kwa Samuel Afful aliyeingia kipindi cha pili.
Pamoja na magoli hayo 4, Azam walikuwa wana uwezo wa kufunga mabao mengi kwani walipata nafasi nzuri za wazi, na wakashindwa kuzitumia vizuri. Nahodha wa Azam, John Bocco alipata nafasi 3 za wazi akashindwa kufunga, na Sure boy alifanikiwa kuwatoka walinzi (mabeki) wa Yanga lakini alishindwa kufunga
Kwa matokeo hayo, Azam wanaongoza kundi B katika michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi, wakifuatiwa na Yanga ambapo wote wana jumla ya pointi 8 ila wanatofautiana kwa kumla ya magoli.
Nusu Fainali ya kwanza itawakutanisha Azam FC na Taifa Jang'ombe, ambapo nusu fainali ya pili itawakutanisha watani wa Jadi (Simba Sc na Yanga), na michezo yote hiyo itachezwa katika uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Unguja, Zanzibar.
Related Articles
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...
Habari nyingine
URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup
Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment