Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Vodacom
Bado tunaendelea na somo letu la data configurations kwa simu za Android zinazotumia laini za mitandao ya simu za mikononi za Tanzania, na somo la leo litajikita katika Mtandao wa Vodacom.
Ukitaja neno Vodacom, hata motto mdogo mwenye ufahamu wake lazima atajua unaizungumzia kampuni kubwa nchini Tanzania inayotoa huduma za mawasiliano ya simu za mikononi. Kampuni hii ipo sokoni kwa muda mrefu, kwa hiyo kwa sasa ina wateja wengi sana. Idadi ya wateja ilionao inatokanana huduma zake nzuri za kupiga simu pamoja na data
Leo tutaangalia namna ya kufanya data Configurations kwenye simu yenye Android OS, inayotumia laini ya mtandao wa Vodacom. Fuata hatua rahisi zifuatazo:
- Hakikisha simu yako umeiwasha
- Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
- Bofya Settings
- Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
- Bofya Access Point Names (APN) Kama simu ina inatumia laini mbili (Dual SIM), chagua laini unayotaka kuifanyia configuration kwa kubofya kwenye jina lake
- Bofya kwenye kitufe cha menu ya simu yako kilichopo chini ya kioo cha smartphone yako, au kinaweza kuwa juu kulia mwa kioo cha simu kutegemeana na aina ya simu.
-
Chagua New APN kisha jaza taarifa kwenye visanduku vya maandishi kama nilivyoainisha hapo chini.
Name: VODACOM
APN: internet
APN type: default
Authentification type: PAP, CHAP, PAP or CHAP, None
Ufafanuzi
Kama unavyoona hapo juu maandishi unayoingiza hakikisha yanakaa katika mpangilio huo. Unapotakiwa kuandika herufi ndogo andika herufi ndogo na unapotakiwa kujaza herufi kubwa jaza herufi kubwa kwani kinyume chake simu yako haitaungwa kwenye Internet.Kwenye Name jaza VODACOM kwa herufi kubwa. Kwenye APN jaza internet na herufi zote ziwe ndogo. Kwenye APN type jaza au chagua default kwa herufi ndogo. Kwenye Authentification type chagua yoyote katika listi inayokuja: PAP or CHAP, nk.
Baada ya kujaza taarifa zinazohitajika kwa usahihi, bofya tena kwenye menu ya simu yako Chagua Save
Sasa waweza kuwasha Data uanze kufurahia ulimwengu wa internet kwa kutumia simu yako kupitia laini ya Vodacom. Kwa maswali au msaada zaidi unaweza kunipigia simu kupitia 0655251774
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment