Nini maana ya 3G?
Neno 3G limeibua mijadala mingi sana katika jamii zetu, ambapo watu wanadadisi wakihitaji kujua maana halisi ya 3G kuanzia tafsiri hadi matumizi au utendaji kazi wake.
Tafsiri ya neno 3G ni rahisi sana katika maisha ya kijamii, lakini katika ufafanuzi wa namna huduma ya 3G inavyofanyakazi ni mgumu kiasi kwamba ukijaribu kufanya utafiti kwenye tovuti mbalimbali utagundua kila tovuti imetoa ufafanuzi tofauti na nyingine japokuwa mada ni moja.
Nzegamedia tumeona kuna haja ya kuchangia machache tunayoyafahamu kuhusu huduma hii inayopendwa zaidi katika zama hizi hususan kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kama vile simu za mikononi, whatsapp, facebook, twitter, instagram, nk. Nakuomba usikimbie; twende sambamba hapo chini:
3G ni neno linalomaanisha kizazi cha tatu katika teknolojia ya mawasiliano ya simu bila waya, kwa kuzingatia viwango vya simu za mikononi vilivyowekwa na umoja wa kimataifa unaosimamia mawasiliano (ITU). Kirefu cha 3G ni ‘Third Generation’. Kirefu cha ITU ni International Telecommunication Union.
Teknolojia ya 3G inatoa huduma ya utumaji wa taifa kwa kiwango cha 200kb kwa sekunde, kiwango ambacho nikikubwa sana kikilinganishwa na teknolojia ya 2G.
Historial ya 3G
Jitihada kutoka kwa wataalamu wa mawasiliano za kuboresha kasi ya mtandao wa Intaneti ilianza zamani lakini nchi ya kwanza kufikia mafanikio ya kupata huduma ya 3G ilikuwa Japan mnamo mwaka 2001. Mwaka 2002, wakorea walianza kutumia huduma ya 3G.Kampuni ya kwanza kupeleka huduma ya mtandao wa 3G nchini Marekani ni Monet Mobile Networks lakini baadae kampuni hiyo ilisitisha huduma zake, lakini mwaka 2002 kampuni nyingine inayojulikana kwa jina la Verizon Wireless iliweza kurudisha huduma ya 3G nchini humo.
Maboresho ya 3G yalipitia hatua mbalimbali na kila hatua ilipewa jina lake kulingana na kasi yake. Majina hayo ya 3G ni 3.5G na 3.75G ambapo kasi iliongezeka kwa kiasi Fulani.
Huduma ya 3G imeanza kutumika hapa nchini kwetu miaka ya hivi karibuni ambapo kwa sasa kampuni zote za simu za mkononi nchini zinatoa huduma hiyo. Mitandao inayotoa huduma hiyo ni pamoja na Tigo, Vodacom, Zantel, Airtel pamoja na Halotel.
Huduma ya 3G huyasaidia makumpuni yanayotoa huduma za simu za mkononi (mobile operators) kutoa huduma nzuri zaidi kwa wateja ikiwa ni pamoja na vifurushi vizuri vya Intaneti pamoja na ‘Online banking’.
Leo hii simu nyingi zimewezeshwa kutumia huduma ya 3G, hivyo kufanya idadi ya watumiaji wa Internet kuwa kubwa siku hadi siku.
Ikumbukwe pia kwamba huduma ya 3G huhitaji miundombinu ya 3G (minara ya 3G) iliyowekwa na kampuni za simu za mikononi, kwa hiyo ukiwa katika maeneo yasio na minara ya 3G, huwezi kupata huduma ya 3G, na badala yake utapata huduma ya 2G kama eneo husika lina huduma hiyo hata kama simu yako ina uwezo wa 3G.
Mara nyingi kampuni zinazotoa huduma ya 3G huweka huduma zake katika maeneo yenye watu wengi hususan mijini. Asilimia kubwa ya miji ya Tanzania kwa sasa ina huduma ya 3G, na mingine imeshapiga hatua kwa kuletewa teknolojia ya kizazi cha nne (4G).
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment