We Like Sharing

Wednesday, January 11, 2017

Nini maana ya 2G?

Nini maana ya 2G?

Nini maana ya 2G?

Neno 2G ni kifupi cha mawili (Second Generation) likiwa na maana ya ‘kizazi cha pili’. Kwa hiyo 2G ni kizazi cha pili katika maendeleo ya teknolojia ya simu bila waya (wireless mobile technology), teknolojia ambayo ina uwezo zaidi kuliko ile ya kizazi cha kwanza (1G).

Mtandao wa 2G ulianza kutumika rasmi mnamo mwaka 1991 nchini Finland, na ulianzishwa kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma ya mawasiliano, ambapo badala ya kupiga tu, watumiaji wa simu walianza kufanya huduma nyingine kama vile kutuma jumbe za maandishi na picha.

Hali kadhalika mawasiliano ya watumiaji wa simu za mikononi yalianza kupata kuwa na ulinzi kwa maana ya kuwa mawasiliano yalikuwa yanatoka kwa mtumaji na kumfikia mlengwa bila kuingiliwa na watu wengine.

Teknolojia ya 2G iliweza kutambulisha kwa mara ya kwanza huduma za kutumia Internet kwenye simu, ambapo watu walianza kutumia simu zao kwa ajili ya kutuma E-mail, kuchati na marafiki pamoja na kutafuta habari za matukio mbalimbali kwenye Intaneti.

Japokuwa Teknolojia ya 2G ilianzishwa Ulaya, lakini hivi sasa inatumika katika nchi zaidi ya 180 duniani kote. Faida za 2G ni kwamba simu zinatumia umeme kidogo sana kuliko simu za kizazi cha kwanza (1G cellphones). Pia teknolojia hii ilisaidia kuondoa changamoto iliyokuwepo katika simu za kizazi cha kwanza ya kufanya sauti za wazungumzaji ‘ku-scratch’.

Pamoja na faida zilizopo kwenye mtandao wa 2G, kasoro hazikosekani. Miongoni mwa kasoro zilizopo katika teknolojia ya 2G ni pamoja na Network ya Internet kuwa na kasi ndogo. Mfano, mtu anayetumia simu ya 2G katika huduma za Internet ni tofauti na Yule anayetumia simu zenye kasi za 3G, 4G, n.k.

Nitajuaje kama simu yangu inatumia mtandao wa 2G? Hili ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa sana na wateja nikiwa katika biashara za Simu na huduma nyingine za simu za mikononi.

Waweza kufahamu kama simu yako ina uwezo wa 2G, kwa kuwasha Data/Internet, kisha uangalie upande wa juu ya kioo, utaona herufi 2G, E au Edge.

Kwa simu za kisasa (smartphones) huwa zina teknolojia mbili au 3 kwa ajili kumpa nafasi mtumiaji kuchagua teknolojia anayotaka kutumia kwa wakati huo, teknolojia hizo ni 2G, 3G, 4G au 5G na uwepo wake kwenye simu unategemea pia uwezo wa simu ya mtumiaji. Kila smartphone inaweza kutumia mtandao wa 2G.

Related Articles

Kulazimisha simu yako isome 4G tu

Internet Configurations za Tigo

4G LTE ni nini?

Internet Configurations za Vodacom

Kulazimisha simu isome 3G tu

Internet Configurations za Halotel

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment