Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Tigo
Asante sana ndugu msomaji kwa kuwa pamoja nasi hapa Nzegamedia. Lengo na mipango yetu ni kuwarahisishia watu katika swala zima la utatuzi wa changamoto zinazowakabili wanapotumia simu zao za mikononi.
Leo tutazungumzia namna ya kufanya Handset Configyurations kwenye simu ya Andorid inayotumia laini ya mtandao wa Tgo. Kwa wale wasiofahamu maana ya Handset configurations, nitawafafanulia kidogo ili nikizama ndani ya somo nisiwatupe mbali wakanilaani kwa kuwapotezea muda, ila kwa unayefahamu maana, waweza kushuka chini moja kwa moja hadi kwenye somo letu la leo.
Handset Configurations ni kitendo cha kuruhusu simu iweze kutumia mobile data pamoja na kuiwezesha kuwasiliana na vifaa vingine vilivyopo katika umbali tofauti wa kijiografia, kama vile computer na simu nyingine kwa kutumia internet ya mtandao wa simu za mkononi.
Simu ambayo haina data configurations zinazokubaliwa na mtandao husika, haiwezi kuwa na Internet access hivyo mtumiaji hawezi kufurahia ulimwengu wa Internet, kama vile kuchati, kutuma email, pamoja na huduma nyingine zinazohitaji internet.
Zifuatazo ni hatua za kufanya Data configurations kwenye simu za Android zinazotumia laini za mtandao wa tigo.
- Hakikisha simu yako umeiwasha
- Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
- Bofya Settings
- Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
- Bofya Access Point Names (APN) Kama simu ina inatumia laini mbili (Dual SIM), chagua laini unayotaka kuifanyia configuration kwa kubofya kwenye jina lake
- Bofya kwenye kitufe cha menu ya simu yako kilichopo chini ya kioo cha smartphone yako, au kinaweza kuwa juu kulia mwa kioo cha simu kutegemeana na aina ya simu.
-
Chagua New APN kisha jaza taarifa kwenye visanduku vya maandishi kama nilivyoainisha hapo chini.
Name: TIGO
APN: tigoweb
APN type: default
Server: http://www.google.com
Authentification type: PAP, CHAP, PAP or CHAP, None
Ufafanuzi
Kama unavyoona hapo juu maandishi unayoingiza hakikisha yanakaa katika mpangilio huo. Unapotakiwa kuandika herufi ndogo andika herufi ndogo na unapotakiwa kujaza herufi kubwa jaza herufi kubwa kwani kinyume chake simu yako haitaungwa kwenye Internet.Kwenye Name jaza TIGO kwa herufi kubwa. Kwenye APN jaza tigoweb na herufi zote ziwe ndogo. Kwenye APN type jaza au chagua default kwa herufi ndogo. Kwenye server si lazima sana kujaza URL ya Google kwa hiyo unaweza kupaacha wazi. Kwenye Authentification type chagua yoyote katika listi inayokuja: PAP or CHAP.
Baada ya kujaza taarifa zinazohitajika kwa usahihi, bofya tena kwenye menu ya simu yako Chagua Save
Sasa waweza kuwasha Data uanze kufurahia ulimwengu wa internet kwa kutumia simu yako kupitia laini ya Tigo. Kwa maswali au msaada zaidi unaweza kunipigia simu kupitia 0655251774
Related Articles
Habari za michezo
Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017
Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC
Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup
Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe
Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup
No comments:
Post a Comment