We Like Sharing

Wednesday, January 11, 2017

Azam yafuzu kwenda fainali ya Kombe la Mapinduzi

Azam yafuzu kwenda fainali ya Kombe la Mapinduzi

Azam yafuzu kwenda fainali ya Kombe la Mapinduzi

Zanzibar, Tanzania

Timu ya Azam FC, almaarufu 'wanalambalamba', imefuzu kwenda fainali katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa timu ya Taifa Jang'ombe ya Unguja, katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa leo jioni katika dimba la Amaan, Zanzibar.

Azam walifanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuitandika Yanga, mabao 4-0 katika mchezo waliocheza tarehe 7/1/2017 katika uwanja wa Amaan, mjini Unguja, ambapo walifanikiwa kupaa hadi kileleni mwa kundi B kwa kuwa na jumla ya pointi 8, wakiwashusha Yanga hadi nafasi ya pili kutoka ya kwanza.

Azam walifanikiwa kupata bao la kwanza na la ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Taifa jan'ombe kunako dakika ya 33 ya kipindi cha kwanza, kupitia kwa Domayo amabaye aliachia shuti kali kuelekea katika lango la timu ya vijana wa Jang'ombe akiwa katika umbali wa mita 19.

Hadi kipenga cha mapumziko kinapulizwa kwa ajili ya mapumziko, Azam walikuwa wanaongoza mchezo kwa bao 1-0.

Katika kipindi cha pili Azam walendeleza mashambulizi kuelekea katika timu ya Taifa Jang'ombe, lakini mashambulizi hayo hayakuzaa matunda kutokana na safu ya ulinzi ya Taifa Jang'ombe kuwa imara zaidi.

Hadi kipenga cha kumaliza mchezo kinapulizwa, Azam walikuwa wanaongoza mchezo kwa bao 1-0, na bao hilo pekee ndio limewapatia wnalambalamba tiketi ya kwenda fainali ya mashindano ya Mapinduzi Cup. Azam wametangulia fainali wakiisubiri timu itakayoshinda mtanange wa leo usiku kati ya Simba SC na Dar Young Africans. Kwa upande mwingine, vijana wa Taifa Jang'ombe wameyaaga mashindano hayo baada ya kipigo cha leo kutoka kwa Azam FC. Pamoja na Taifa jang'ombe kutolewa katika michuano hiyo, wameondoka na sifa nzuri ya kucheza michezo mizuri, kwani ni miongoni mwa timu za visiwani Zanzibar zilizokuwa zikivipa presha vilabu vya Tanzania bara vilivyoshiriki mashindano hayo 2017.

Related Articles

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Simba Sports Club, almaarufu wazee wa msimbazi wameianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar 2017, baada ya kuicharanga mabao 2-1 klabu ya Taifa Jang'ombe. Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan usiku huu mjini Unguja, ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu ya Simba tangu kuanza kwa michuano ya kombe hilo tarehe 30/12/2016...

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

Timu ya Yanga almaarufu wakimataifa, wameianza vizuri michuano ya Mapinduzi Cup 2017, inayofanyika kila mwaka mjini Zanzibar, baada ya kuwachapa mabao 6-0 walima karafuu wa Pemba, Jamhuri, katika mchezo uliopigwa usiku huu kwenye uwanja wa Amaan uliopo katikati ya mji wa Zanzibar...

Habari nyingine

URA yashindwa kutamba mbele ya Simba SC, Mapinduzi Cup

Azam FC yalazimishwa sare na Jamhuri FC ya Pemba

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment