We Like Sharing

Wednesday, January 11, 2017

Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Airtel

Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Airtel

Kufanya Internet Configurations kwenye android yenye laini ya Airtel

Nzegamedia tunaendelea kukupatia elimu ya teknolojia bila malipo, na kutokana na maombi ya wasomaji wetu, waliomba tuchapishe pia masomo yetu kwa Lugha ya Kiswahili badala ya kiingereza pekee, hivyo bila hiana tumepokea maombi yao na tumeshachukua hatua.

Katika somo lililopita tulijifunza namna ya kufanya Handset Configuration kwenye simu za Android zinazotumia laini za mtandao wa Halotel. Kwa wale waliopata nafasi ya kusoma, naimani walijinza kitu.

Somo la leo tutajikita katika mtandao wa Airtel, ambapo tutajifunza namna ya kufanya Data Configurations kwa simu za Android zinazotumia laini za Airtel. Airtel ni mtandao kongwe ambao umekuwepo katika soko la huduma za simu za mkononi hapa nchini kwa zaidi ya muongo mmoja.

Tokea kipindi mtandao huu ukijulikana kwa jina la Celtel, Zain hadi leo ambapo unajulikana kwa jina la Airtel. Kama una laini ya laini ya Airtel kwenye simu yako inayotumia Operating system ya Android, na unahitaji kutumia internet yake, fuata hatua rahisi zifuatazo:

  1. Hakikisha simu yako umeiwasha
  2. Bofya kwenye menu kuu ya simu yako
  3. Bofya Settings
  4. Katika sehemu ya Wireless & Networks bofya Mobile Networks. Kama neno Mobile networks halipo, chagua More kisha utaiona option hiyo ya Mobile Netwotks kutegemeana na aina ya simu yako au toleo la Android Operating system iliyowekwa kwenye simu yako.
  5. Bofya Access Point Names (APN) Kama simu ina inatumia laini mbili (Dual SIM), chagua laini unayotaka kuifanyia configuration kwa kubofya kwenye jina lake
  6. Bofya kwenye kitufe cha menu ya simu yako kilichopo chini ya kioo cha smartphone yako, au kinaweza kuwa juu kulia mwa kioo cha simu kutegemeana na aina ya simu.
  7. Chagua New APN kisha jaza taarifa kwenye visanduku vya maandishi kama nilivyoainisha hapo chini.
    Name: AIRTEL
    APN: internet
    APN type: default
    Authentification type: PAP, CHAP, PAP or CHAP, None

Ufafanuzi

Kama unavyoona hapo juu maandishi unayoingiza hakikisha yanakaa katika mpangilio huo. Unapotakiwa kuandika herufi ndogo andika herufi ndogo na unapotakiwa kujaza herufi kubwa jaza herufi kubwa kwani kinyume chake simu yako haitaungwa kwenye Internet.

Kwenye Name jaza AIRTEL kwa herufi kubwa. Kwenye APN jaza internet na herufi zote ziwe ndogo. Kwenye APN type jaza au chagua default kwa herufi ndogo. Kwenye Authentification type chagua yoyote katika listi inayokuja: PAP or CHAP, nk.

Baada ya kujaza taarifa zinazohitajika kwa usahihi, bofya tena kwenye menu ya simu yako Chagua Save

Sasa waweza kuwasha Data uanze kufurahia ulimwengu wa internet kwa kutumia simu yako kupitia laini ya Airtel. Kwa maswali au msaada zaidi unaweza kunipigia simu kupitia 0655251774

Related Articles

Internet Configurations za Zantel

Internet Configurations za Tigo

3G ni nini na inafanyaje kazi?

Internet Configurations za Vodacom

Kampuni kubwa zinazotengeneza Smartphones

Internet Configurations za Halotel

Habari za michezo

Timu zinazoshiriki Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2017

Yanga yaichapa 2-0 Zimamoto FC

Simba SC yazidi kusonga mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup

Simba SC yailambisha mabao 2-1 timu ya Taifa Jang'ombe

Yanga yaichapa Jamhuri mabao 6-0 katika michuano ya Mapinduzi Cup

©2016. Nzegamedia! Designed by Chris Kabeya De Pro

No comments:

Post a Comment